Joshua 20:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwuaji ataendelea kuishi humo mpaka hapo atakapohukumiwa mbele ya jumuiya nzima ya Israeli na pia mpaka hapo yule kuhani mkuu ambaye alikuwa na madaraka wakati huo amefariki. Baada ya hapo mtu huyo ataweza kurudi nyumbani kwake katika mji ule alikotoroka.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huyu aliyeua atakaa kwenye mji huo hadi awe amesimama kukabili mashtaka yake mbele ya kusanyiko na hadi kuhani mkuu anayehudumu kwa wakati huo atakapokufa. Ndipo atakapoweza kurudi nyumbani mwake katika mji ambao aliukimbia.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye atakaa katika mji huo, hata hapo atakaposimama mbele ya mkutano kuhukumiwa, hata kifo chake kuhani mkuu mwenye kuwapo siku hizo; ndipo yule mwuaji atarudi, na kuuendea mji wake mwenyewe, na nyumba yake mwenyewe, hata mji huo alioutoka hapo alipokimbia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwuaji ataendelea kuishi humo mpaka hapo atakapohukumiwa mbele ya jumuiya nzima ya Israeli na pia mpaka hapo yule kuhani mkuu ambaye alikuwa na madaraka wakati huo amefariki. Baada ya hapo mtu huyo ataweza kurudi nyumbani kwake katika mji ule alikotoroka.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huyu aliyeua atakaa kwenye mji huo mpaka awe amesimama kukabili mashtaka yake mbele ya kusanyiko na mpaka Kuhani Mkuu anayehudumu kwa wakati huo atakapokufa. Ndipo atakapoweza kurudi nyumbani kwake katika mji ambao aliukimbia.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huyu aliyeua atakaa kwenye mji mkubwa huo mpaka awe amesimama kukabili mashtaka yake mbele ya kusanyiko na mpaka kuhani mkuu anayehudumu kwa wakati huo atakapokufa. Ndipo atakapoweza kurudi nyumbani kwake katika mji ambao aliukimbia.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye atakaa katika mji huo, hadi hapo atakaposimama mbele ya mkutano kuhukumiwa, hadi kifo chake kuhani mkuu mwenye kuwapo siku hizo; ndipo yule mwuaji atarudi, na kuuendea mji wake mwenyewe, na nyumba yake mwenyewe, hadi mji huo aliyoutoka hapo alipokimbia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwuaji ataendelea kuishi humo mpaka hapo atakapohukumiwa mbele ya jumuiya nzima ya Israeli na pia mpaka hapo yule kuhani mkuu ambaye alikuwa na madaraka wakati huo amefariki. Baada ya hapo mtu huyo ataweza kurudi nyumbani kwake katika mji ule alikotoroka.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye atakaa humo mjini, mpaka atakaposimamishwa mbele ya mkutano, apate kuhukumiwa, tena mpaka mtambikaji mkuu wa siku zile atakapokufa, kisha yule mwuaji atapata kurudi na kuingia mjini kwao na nyumbani mwao mlemle mjini, alimotoka na kukimbia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye atakaa katika mji huo, hata hapo atakaposimama mbele ya mkutano kuhukumiwa, hata kifo chake kuhani mkuu mwenye kuwapo siku hizo; ndipo yule mwuaji atarudi, na kuuendea mji wake mwenyewe, na nyumba yake mwenyewe, hata mji huo alioutoka hapo alipokimbia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mwuaji ataendelea kuishi mule mpaka pale atakapohukumiwa mbele ya mukutano wote wa Waisraeli na vilevile mpaka pale yule Kuhani Mukubwa ambaye alikuwa na madaraka wakati ule atakapokufa. Nyuma ya pale mutu huyo ataweza kurudi katika nyumba yake katika muji ule pahali alipotoka wakati alipotoroka.”