Joshua 20:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Katika ngambo ya mto Yordani, mashariki ya mji wa Yeriko, walichagua mji wa Bezeri ulio kwenye nyika tambarare na ambao mji wenyewe ni wa eneo la kabila la Reubeni. Pia walichagua Ramothi huko Gileadi ambao ni mji wa kabila la Gadi na Golani huko Bashani katika eneo la kabila la Manase.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika upande wa mashariki mwa Yordani (ng’ambo ya Yeriko) wakatenga Bezeri katika jangwa katika uwanda wa juu katika kabila la Reubeni, Ramothi katika Gileadi katika kabila la Gadi, na Golani huko Bashani katika kabila la Manase.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena ng'ambo ya pili ya Yordani pande za Yeriko upande wa kuelekea mashariki wakaweka Bezeri ulioko nyikani, katika nchi tambarare ya kabila ya Reubeni, na Ramothi katika Gileadi katika kabila ya Gadi, na Golani katika Bashani katika kabila ya Manase.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Katika ng'ambo ya mto Yordani, mashariki ya mji wa Yeriko, walichagua mji wa Bezeri ulio kwenye nyika tambarare na ambao mji wenyewe ni wa eneo la kabila la Reubeni. Pia walichagua Ramothi huko Gileadi ambao ni mji wa kabila la Gadi na Golani huko Bashani katika eneo la kabila la Manase.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika upande wa mashariki ya Yordani ya Yeriko wakatenga Bezeri katika jangwa katika uwanda wa juu katika kabila la Reubeni, Ramoth katika Gileadi katika kabila la Gadi, na Golani huko Bashani katika kabila la Manase.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika upande wa mashariki mwa Yordani ya Yeriko wakatenga Bezeri katika jangwa katika uwanda wa juu katika kabila la Reubeni, Ramothi katika Gileadi katika kabila la Gadi, na Golani huko Bashani katika kabila la Manase.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena ng'ambo ya pili ya Yordani pande za Yeriko upande wa kuelekea mashariki wakaweka Bezeri ulioko nyikani, katika nchi tambarare ya kabila la Reubeni, na Ramothi katika Gileadi katika kabila la Gadi, na Golani katika Bashani katika kabila la Manase.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Katika ngambo ya mto Yordani, mashariki ya mji wa Yeriko, walichagua mji wa Bezeri ulio kwenye nyika tambarare na ambao mji wenyewe ni wa eneo la kabila la Reubeni. Pia walichagua Ramothi huko Gileadi ambao ni mji wa kabila la Gadi na Golani huko Bashani katika eneo la kabila la Manase.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena ng'ambo ya huko ya Yordani upande wa Yeriko wa Maawioni kwa jua wakatoa kwa shina la Rubeni mji wa Beseri ulioko nyikani juu mlimani panapokwenda sawa, tena Ramoti wa Gileadi kwa shina la Gadi na Golani wa Basani kwa shina la Manase.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena ng’ambo ya pili ya Yordani pande za Yeriko upande wa kuelekea mashariki wakaweka Bezeri ulioko nyikani, katika nchi tambarare ya kabila ya Reubeni, na Ramothi katika Gileadi katika kabila ya Gadi, na Golani katika Bashani katika kabila ya Manase.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na ngambo ya muto Yordani, upande wa mashariki wa muji wa Yeriko, walichagua muji wa Bezeri unaokuwa kwenye jangwa katika mabonde ya eneo la kabila la Rubeni. Vilevile wakachagua Ramoti, kule Gileadi ambao ni muji wa kabila la Gadi na Golani kule Basani katika eneo la kabila la Manase.