Joshua 20:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hii ndiyo miji iliyotengwa kwa ajili ya watu wote wa Israeli na wageni walioishi miongoni mwao, ili mtu yeyote atakayemuua mwenzake bila kukusudia akimbilie huko asije akauawa na mwenye jukumu la kulipiza kisasi cha damu, hadi hapo atakapohukumiwa mbele ya jumuiya nzima.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwisraeli yeyote au mgeni yeyote aishiye miongoni mwao aliyemuua mtu kwa bahati mbaya, angeweza kukimbilia katika miji hiyo iliyotengwa na asiuawe na mlipiza kisasi wa damu kabla hajasimama kukabili mashtaka mbele ya kusanyiko.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Miji hiyo ndiyo miji iliyoamriwa kwa ajili ya wana wa Israeli wote, na kwa ajili ya mgeni akaaye kati yao ugenini, ili kwamba mtu awaye yote atakayemwua mtu pasipo kukusudia apate kimbilia huko, asife kwa mkono wa mwenye kujilipiza kisasi cha damu, hata hapo atakapokuwa amekwisha simama mbele ya mkutano.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hii ndiyo miji iliyotengwa kwa ajili ya watu wote wa Israeli na wageni walioishi miongoni mwao, ili mtu yeyote atakayemuua mwenzake bila kukusudia akimbilie huko asije akauawa na mwenye jukumu la kulipiza kisasi cha damu, hadi hapo atakapohukumiwa mbele ya jumuiya nzima.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mwisraeli ye yote au mgeni ye yote aishiye miongoni mwao aliyemwua mtu kwa bahati mbaya, angeweza kukimbilia katika miji hiyo iliyotengwa na asiuawe na mwenye kulipiza kisasi cha damu kabla hajasimama kukabili mashtaka mbele ya kusanyiko.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mwisraeli yeyote au mgeni yeyote aishiye miongoni mwao aliyemuua mtu kwa bahati mbaya, angeweza kukimbilia katika miji mikubwa hiyo iliyotengwa na asiuawe na mlipiza kisasi wa damu kabla hajasimama kukabili mashtaka mbele ya kusanyiko.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Miji hiyo ndiyo miji iliyoamriwa kwa ajili ya wana wa Israeli wote, na kwa ajili ya mgeni akaaye kati yao ugenini, ili kwamba mtu yeyote atakayemwua mtu pasipo kukusudia apate kukimbilia huko, asife kwa mkono wa mwenye kujilipiza kisasi cha damu, hadi hapo atakapokuwa amekwisha simama mbele ya mkutano.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hii ndiyo miji iliyotengwa kwa ajili ya watu wote wa Israeli na wageni walioishi miongoni mwao, ili mtu yeyote atakayemuua mwenzake bila kukusudia akimbilie huko asije akauawa na mwenye jukumu la kulipiza kisasi cha damu, hadi hapo atakapohukumiwa mbele ya jumuiya nzima.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hii ndiyo miji iliyowekewa wana wote wa Isiraeli nao wageni waliokaa ugenini kwao ya kuikimbilia; mtu ye yote asiyemwua mwenziwe kwa kusudi asiuawe na mkono wake mwenye kuilipiza hiyo damu, mpaka asimamishwe mbele ya mkutano.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Miji hiyo ndiyo miji iliyoamriwa kwa ajili ya wana wa Israeli wote, na kwa ajili ya mgeni akaaye kati yao ugenini, ili kwamba mtu awaye yote atakayemwua mtu pasipo kukusudia apate kimbilia huko, asife kwa mkono wa mwenye kujilipiza kisasi cha damu, hata hapo atakapokuwa amekwisha simama mbele ya mkutano.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hii ndiyo miji iliyotengwa kwa ajili ya watu wote wa Israeli na wageni walioishi kati yao, kusudi mutu yeyote atakayemwua mwenzake bila kukusudia akimbilie kule asipate kuuawa na mwenye ruhusa ya kulipiza kisasi cha damu, mpaka pale atakapohukumiwa mbele ya mukutano wa watu wote.