Joshua 21:27 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Jamaa za Walawi za ukoo wa Gershoni, walipewa miji miwili katika nusu ya eneo la kabila la Manase: Golani, huko Bashani, mji wa kukimbilia usalama, pamoja na mbuga zake za malisho, na Beesh-tera pamoja na malisho yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Koo za Walawi za Wagershoni walipewa: kutoka nusu ya kabila la Manase: Golani katika Bashani (mji wa makimbilio kwa yeyote aliyeshtakiwa kwa mauaji) na Beeshtera, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji: miji miwili;
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena wana wa Gershoni, katika jamaa za Walawi, waliwapa, katika hiyo nusu ya kabila ya Manase, Golani katika Bashani pamoja na malisho yake, huo mji wa makimbilio kwa ajili ya mwuaji; na Beeshtera pamoja na malisho yake; miji miwili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Jamaa za Walawi za ukoo wa Gershoni, walipewa miji miwili katika nusu ya eneo la kabila la Manase: Golani, huko Bashani, mji wa kukimbilia usalama, pamoja na mbuga zake za malisho, na Beesh-tera pamoja na malisho yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Koo za Walawi za Wagerishoni walipewa: kutoka katika nusu ya Manase, Golani katika Bashani (mji wa makimbilio kwa ye yote aliyeshtakiwa kwa mauaji) na Beeshtera, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji miwili;
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Koo za Walawi za Wagershoni walipewa: kutoka nusu ya kabila la Manase, Golani katika Bashani (mji mkuu wa makimbilio kwa yeyote aliyeshtakiwa kwa mauaji) na Beeshtera, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji miwili;
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena wana wa Gershoni, katika jamaa za Walawi, waliwapa, katika hiyo nusu ya kabila la Manase, Golani katika Bashani pamoja na mbuga zake za malisho, huo mji wa makimbilio kwa ajili ya mwuaji; na Beeshtera pamoja na mbuga zake za malisho; miji miwili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Jamaa za Walawi za ukoo wa Gershoni, walipewa miji miwili katika nusu ya eneo la kabila la Manase: Golani, huko Bashani, mji wa kukimbilia usalama, pamoja na mbuga zake za malisho, na Beesh-tera pamoja na malisho yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao wana wa Gersoni waliokuwa miongoni mwa koo za Walawi walipata kwa nusu ya shina la Manase mji wa Golani huko Basani uliokuwa wa kukimbilia wauaji pamoja na malisho yake na Bestera pamoja na malisho yake, ndio miji 2.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena wana wa Gershoni, katika jamaa za Walawi, waliwapa, katika hiyo nusu ya kabila ya Manase, Golani katika Bashani pamoja na malisho yake, huo mji wa makimbilio kwa ajili ya mwuaji; na Beeshtera pamoja na malisho yake; miji miwili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wa uzao wa Lawi wa ukoo wa Gersoni, walipewa miji miwili katika nusu ya eneo la kabila la Manase: Golani, kule Basani, muji wa kukimbilia usalama, pamoja na mbuga zake za malisho, na Be-Estera pamoja na malisho yake.