Joshua 21:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, kulingana na amri ya Mwenyezi-Mungu, Waisraeli walichagua kutoka katika maeneo ya nchi zao, miji na vijiji vya malisho, wakawapa Walawi iwe sehemu yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo kama vile Mwenyezi Mungu alivyoamuru, Waisraeli wakawapa Walawi miji ifuatayo, na maeneo ya malisho ya kila mji kutoka urithi wao wenyewe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wana wa Israeli wakawapa Walawi miji hii, pamoja na malisho yake, katika urithi wao, sawasawa na hiyo amri ya Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, kulingana na amri ya Mwenyezi-Mungu, Waisraeli walichagua kutoka katika maeneo ya nchi zao, miji na vijiji vya malisho, wakawapa Walawi iwe sehemu yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo kama vile BWANA alivyoagiza, Waisraeli wakawapa Walawi miji ifuatayo pamoja na sehemu zake za malisho kutoka katika urithi wao wenyewe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo kama vile bwana alivyoamuru, Waisraeli wakawapa Walawi miji ifuatayo pamoja na sehemu zake za malisho kutoka urithi wao wenyewe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wana wa Israeli wakawapa Walawi miji hii, pamoja na mbuga zake za malisho, katika urithi wao, sawasawa na hiyo amri ya BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, kulingana na amri ya Mwenyezi-Mungu, Waisraeli walichagua kutoka katika maeneo ya nchi zao, miji na vijiji vya malisho, wakawapa Walawi iwe sehemu yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo wana wa Isiraeli wakawatolea Walawi kwa kuagizwa na Bwana katika mafungu yao miji hii pamoja na malisho yao:
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wana wa Israeli wakawapa Walawi miji hii, pamoja na malisho yake, katika urithi wao, sawasawa na hiyo amri ya BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, kulingana na amri ya Yawe, Waisraeli walichagua kutoka katika maeneo ya inchi zao, miji na vijiji vya malisho, wakawapa Walawi ikuwe sehemu yao.