Joshua 21:32 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Katika eneo la kabila la Naftali walipewa Kedeshi, mji wa kukimbilia usalama ulioko huko Galilaya pamoja na mbuga zake za malisho, Hamoth-dori pamoja na mbuga zake za malisho na Kartani pamoja na mbuga zake za malisho. Jumla miji mitatu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kutoka kabila la Naftali, walipewa: Kedeshi katika Galilaya (mji wa makimbilio kwa ajili ya yeyote anayeshtakiwa kwa mauaji), Hamoth-Dori na Kartani, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji: miji mitano.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena katika kabila ya Naftali, Kedeshi katika Galilaya pamoja na malisho yake, huo mji wa makimbilio kwa ajili ya mwuaji, na Hamoth-dori pamoja na malisho yake, na Kartani pamoja na malisho yake; miji mitatu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Katika eneo la kabila la Naftali walipewa Kedeshi, mji wa kukimbilia usalama ulioko huko Galilaya pamoja na mbuga zake za malisho, Hamoth-dori pamoja na mbuga zake za malisho na Kartani pamoja na mbuga zake za malisho. Jumla miji mitatu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kutoka katika kabila la Naftali walipewa, Kedeshi katika Galilaya (mji wa makimbilio kwa ajili ya ye yote anayeshtakiwa kwa mauaji), Hamoth-Dori na Kartani, yote miji mitano pamoja na sehemu zake za malisho.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kutoka kabila la Naftali walipewa, Kedeshi katika Galilaya (mji wa makimbilio kwa ajili ya yeyote anayeshtakiwa kwa mauaji), Hamoth-Dori na Kartani, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji mitano.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena katika kabila la Naftali, Kedeshi katika Galilaya pamoja na mbuga zake za malisho, huo mji wa makimbilio kwa ajili ya mwuaji, na Hamoth-dori pamoja na mbuga zake za malisho, na Kartani pamoja na mbuga zake za malisho; miji mitatu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Katika eneo la kabila la Naftali walipewa Kedeshi, mji wa kukimbilia usalama ulioko huko Galilaya pamoja na mbuga zake za malisho, Hamoth-dori pamoja na mbuga zake za malisho na Kartani pamoja na mbuga zake za malisho. Jumla miji mitatu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena kwa shina la Nafutali: mji wa Kedesi uliokuwa wa kukimbilia wauaji kule Galili pamoja na malisho yake na Hamoti-Dori pamoja na malisho yake na Kartani pamoja na malisho yake, ndio miji 3.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena katika kabila ya Naftali, Kedeshi katika Galilaya pamoja na malisho yake, huo mji wa makimbilio kwa ajili ya mwuaji, na Hamoth-dori pamoja na malisho yake, na Kartani pamoja na malisho yake; miji mitatu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika eneo la kabila la Nafutali walipewa Kedesi, muji wa kukimbilia usalama unaokuwa kule Galilaya pamoja na mbuga zake za malisho, Hamoti-Dori pamoja na mbuga zake za malisho na Kartani pamoja na mbuga zake za malisho. Kwa jumla, miji mitatu.