Joshua 21:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kura ya kwanza ilizipata jamaa za ukoo wa Kohathi. Miongoni mwao wazawa wa kuhani Aroni walipewa kwa kura, miji iliyokuwa katika maeneo ya makabila ya Yuda, Simeoni, na Benyamini. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na mitatu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kura ya kwanza ikaangukia Wakohathi, kufuatana na koo zao. Walawi waliokuwa wazao wa kuhani Haruni walipewa miji kumi na tatu kutoka makabila ya Yuda, Simeoni na Benyamini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kura ikatokea kwa ajili ya jamaa za Wakohathi; na wana wa Haruni kuhani, waliokuwa katika Walawi, walipata miji kumi na mitatu kwa kura katika kabila ya Yuda, na katika kabila ya Simeoni, na katika kabila ya Benyamini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kura ya kwanza ilizipata jamaa za ukoo wa Kohathi. Miongoni mwao wazawa wa kuhani Aroni walipewa kwa kura, miji iliyokuwa katika maeneo ya makabila ya Yuda, Simeoni, na Benyamini. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na mitatu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kura ya kwanza ikatoka kwa ajili ya Wakohathi, ukoo kwa ukoo. Walawi waliokuwa wazao wa kuhani Aroni walipewa miji kumi na mitatu kutoka katika makabila ya Yuda, Simeoni na Benyamini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kura ya kwanza ikaangukia Wakohathi, ukoo kwa ukoo. Walawi waliokuwa wazao wa kuhani Haruni walipewa miji kumi na mitatu kutoka makabila ya Yuda, Simeoni na Benyamini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kura ikatokea kwa ajili ya jamaa za Wakohathi; na wana wa Haruni kuhani, waliokuwa katika Walawi, walipata miji kumi na mitatu kwa kura katika kabila la Yuda, na katika kabila la Simeoni, na katika kabila la Benyamini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kura ya kwanza ilizipata jamaa za ukoo wa Kohathi. Miongoni mwao wazawa wa kuhani Aroni walipewa kwa kura, miji iliyokuwa katika maeneo ya makabila ya Yuda, Simeoni, na Benyamini. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na mitatu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Koo za Wakehati zilipopigiwa kura, wana wa mtambikaji Haroni waliokuwa katika hawa Walawi walipata miji 13 kwa shina la Yuda na kwa shina la Simeoni na kwa shina la Benyamini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kura ikatokea kwa ajili ya jamaa za Wakohathi; na wana wa Haruni kuhani, waliokuwa katika Walawi, walipata miji kumi na mitatu kwa kura katika kabila ya Yuda, na katika kabila ya Simeoni, na katika kabila ya Benyamini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kura ya kwanza ilizipata jamaa za ukoo wa Kohati. Kati ya wazao wa kuhani Haruni walipewa kwa kura, miji iliyokuwa katika maeneo ya makabila ya Yuda, Simeoni, na Benjamina. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na mitatu.