Joshua 21:41 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Jumla ya miji yote ambayo Walawi walipewa katika maeneo ya Waisraeli ilikuwa arubaini na minane pamoja na mbuga zao za malisho.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Miji yote ya Walawi katika eneo lililomilikiwa na Waisraeli ilikuwa arobaini na nane, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Miji yote ya Walawi iliyokuwa kati ya milki ya wana wa Israeli ilikuwa ni miji arobaini na minane, pamoja na malisho yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Jumla ya miji yote ambayo Walawi walipewa katika maeneo ya Waisraeli ilikuwa arubaini na minane pamoja na mbuga zao za malisho.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Miji yote ya Walawi katika nchi iliyoshikwa na Waisraeli ilikuwa arobaini na minane, pamoja na sehemu zake za malisho.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Miji yote ya Walawi katika eneo lililoshikwa na Waisraeli lilikuwa arobaini na minane, pamoja na sehemu zake za malisho.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Miji yote ya Walawi iliyokuwa kati ya milki ya wana wa Israeli ilikuwa ni miji arobaini na minane, pamoja na mbuga zake za malisho.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Jumla ya miji yote ambayo Walawi walipewa katika maeneo ya Waisraeli ilikuwa arubaini na minane pamoja na mbuga zao za malisho.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Miji yote ya Walawi iliyokuwa katikati ya nchi zao wana wa Isiraeli ilikuwa miji 48 pamoja na malisho yao yaliyoizunguka;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Miji yote ya Walawi iliyokuwa kati ya milki ya wana wa Israeli ilikuwa ni miji arobaini na minane, pamoja na malisho yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Jumla ya miji yote ambayo Walawi walipewa katika maeneo ya Waisraeli ilikuwa makumi ine na nane pamoja na mbuga zao za malisho.