Joshua 22:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, habari zikawafikia watu wa makabila mengine ya Israeli kwamba makabila ya Reubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase yalikuwa yamejenga madhabahu kubwa karibu na mto Yordani katika nchi ya Kanaani, yaani ndani ya eneo lao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waisraeli hao wengine waliposikia kwamba Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase walikuwa wamejenga madhabahu kwenye mpaka wa Kanaani huko Gelilothi karibu na Yordani kwenye upande wa Israeli,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wana wa Israeli walisikia ikinenwa, Tazama, wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na hiyo nusu ya kabila ya Manase, wamejenga madhabahu huko upande wa mbele wa nchi ya Kanaani, katika nchi iliyo karibu na Yordani, kwa upande huo ulio milki ya wana wa Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, habari zikawafikia watu wa makabila mengine ya Israeli kwamba makabila ya Reubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase yalikuwa yamejenga madhabahu kubwa karibu na mto Yordani katika nchi ya Kanaani, yaani ndani ya eneo lao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wale Waisraeli wengine waliposikia kwamba Wareubeni, Wagadi na ile nusu ya kabila la Manase walikuwa wamejenga madhabahu upande wa magharibi mwa Yordani kwenye mpaka wa Kanaani huko Gelilothi,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waisraeli wengine waliposikia kwamba Wareubeni, Wagadi na ile nusu ya kabila la Manase walikuwa wamejenga madhabahu kwenye mpaka wa Kanaani huko Gelilothi karibu na Yordani kwenye upande wa Israeli,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wana wa Israeli walisikia ikinenwa, Tazama, wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na hiyo nusu ya kabila la Manase, wamejenga madhabahu huko upande wa mbele wa nchi ya Kanaani, katika nchi iliyo karibu na Yordani, kwa upande huo ulio milki ya wana wa Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, habari zikawafikia watu wa makabila mengine ya Israeli kwamba makabila ya Reubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase yalikuwa yamejenga madhabahu kubwa karibu na mto Yordani katika nchi ya Kanaani, yaani ndani ya eneo lao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wana wa Isiraeli waliposikia kwamba: Tazameni, wana wa Rubeni na wana wa Gadi nao wale wa nusu ya shina la Manese wamejenga pa kutambikia upande wa kwao wa kuielekea nchi ya Kanaani katika majimbo ya Yordani ng'ambo ya huko, wana wa Isiraeli wapaone,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wana wa Israeli walisikia ikinenwa, Tazama, wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na hiyo nusu ya kabila ya Manase, wamejenga madhabahu huko upande wa mbele wa nchi ya Kanaani, katika nchi iliyo karibu na Yordani, kwa upande huo ulio milki ya wana wa Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, habari zikawafikia watu wa makabila mengine ya Israeli kwamba makabila ya Rubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase yalikuwa yamejenga mazabahu kubwa karibu na muto Yordani katika inchi ya Kanana, ni kusema ndani ya eneo lao.