Joshua 22:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, watu wa Israeli wakamtuma Finehasi, mwanawe kuhani Eleazari, huko Gileadi kwa makabila ya Reubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo Waisraeli wengine wakamtuma Finehasi, mwana wa kuhani Eleazari, aende katika nchi ya Gileadi kwa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha wana wa Israeli wakatuma wajumbe waende kwa wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na hiyo nusu ya kabila ya Manase, hata nchi ya Gileadi; nao ni hawa, Finehasi mwana wa Eleazari kuhani;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, watu wa Israeli wakamtuma Finehasi, mwanawe kuhani Eleazari, huko Gileadi kwa makabila ya Reubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo hao Waisraeli wengine wakamtuma Finehasi mwana wa kuhani Eleazari katika nchi ya Gileadi, aende kwa Wareubeni, Wagadi na hiyo nusu ya kabila la Manase.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo Waisraeli wengine wakamtuma Finehasi mwana wa kuhani Eleazari katika nchi ya Gileadi, kwa Wareubeni, Wagadi na hiyo nusu ya kabila la Manase.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha wana wa Israeli wakatuma wajumbe waende kwa wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na hiyo nusu ya kabila la Manase, hadi nchi ya Gileadi; nao ni hawa, Finehasi mwana wa Eleazari kuhani;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, watu wa Israeli wakamtuma Finehasi, mwanawe kuhani Eleazari, huko Gileadi kwa makabila ya Reubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini kwanza wana wa Isiraeli wakatuma wajumbe kwa wana wa Rubeni na kwa wana wa Gadi na kwa wale wa nusu ya shina la Manese katika nchi ya Gileadi; waliotumwa ni Pinehasi, mwana wa mtambikaji Elazari,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha wana wa Israeli wakatuma wajumbe waende kwa wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na hiyo nusu ya kabila ya Manase, hata nchi ya Gileadi; nao ni hawa, Finehasi mwana wa Eleazari kuhani;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, watu wa Israeli wakamutuma Finehasi mwana wa kuhani Eleazari, kule Gileadi kwa makabila ya Rubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase.