Joshua 22:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Jumuiya nzima ya Mwenyezi-Mungu inauliza hivi: ‘Ni udanganyifu gani huu mmemfanyia Mungu wa Israeli? Mbona mmemwasi Mwenyezi-Mungu kwa kujenga madhabahu hii?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kusanyiko lote la Mwenyezi Mungu wasema hivi: ‘Je, mmewezaje kuacha kumwamini Mungu wa Israeli jinsi hii? Mmewezaje kumwacha Mwenyezi Mungu na kujijengea madhabahu dhidi yake na kumwasi?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mkutano wote wa Bwana wanena, Ni kosa gani hili mlilolikosa juu ya Mungu wa Israeli, hata mkakengeuka hivi leo na kuacha kumwandama Bwana, katika kujijengea madhabahu, na kuasi hivi leo juu ya Bwana?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Jumuiya nzima ya Mwenyezi-Mungu inauliza hivi: ‘Ni udanganyifu gani huu mmemfanyia Mungu wa Israeli? Mbona mmemwasi Mwenyezi-Mungu kwa kujenga madhabahu hii?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kusanyiko lote la BWANA lasema: ‘Je, mmewezaje kuacha kumwamini Mungu wa Israeli kwa kufanya jambo kama hili? Mmewezaje kumwacha BWANA na sasa kujijengea madhabahu dhidi yake na kumwasi?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kusanyiko lote la bwana lasema: ‘Je, mmewezaje kuacha kumwamini Mungu wa Israeli jinsi hii? Mmewezaje kumwacha bwana na kujijengea madhabahu dhidi yake na kumwasi?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mkutano wote wa BWANA wanena, Ni kosa gani hili mlilolikosa juu ya Mungu wa Israeli, hata mkakengeuka hivi leo na kuacha kumfuata BWANA, katika kujijengea madhabahu, na kuasi hivi leo juu ya BWANA?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Jumuiya nzima ya Mwenyezi-Mungu inauliza hivi: ‘Ni udanganyifu gani huu mmemfanyia Mungu wa Israeli? Mbona mmemwasi Mwenyezi-Mungu kwa kujenga madhabahu hii?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivi ndivyo, wao wa mkutano wote wa Bwana wanavyosema: Huku kuyavunja maagano, mnayomvunjia Mungu wa Isiraeli, maana yake nini? Mbona sasa mmerudi nyuma na kumwacha Bwana kwa kujijengea pa kutambikia? Basi, hivyo hamkumkataa sasa Mungu mkiacha kumtii?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mkutano wote wa BWANA wanena, Ni kosa gani hili mlilolikosa juu ya Mungu wa Israeli, hata mkakengeuka hivi leo na kuacha kumwandama BWANA, katika kujijengea madhabahu, na kuasi hivi leo juu ya BWANA?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Watu wote wa Yawe wanauliza hivi: ‘Ni udanganyifu gani huu mumemufanyia Mungu wa Israeli? Mbona mumemwasi Yawe kwa kujenga mazabahu hii?