Joshua 22:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa nini, basi, mmeacha kumfuata Mwenyezi-Mungu? Mkimwasi Mwenyezi-Mungu leo, kesho ataikasirikia sana jumuiya nzima ya Israeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, sasa ndiyo mnamwacha Mwenyezi Mungu? “ ‘Mkimwasi Mwenyezi Mungu leo, kesho atawakasirikia kusanyiko lote la Israeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
hata ikawa hamna budi hivi leo kugeuka na kuacha kumwandama Bwana? Kisha itakuwa, kwa kuwa ninyi mwamwasi Bwana hivi leo, kwamba kesho yeye atakasirika na mkutano wote wa Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa nini, basi, mmeacha kumfuata Mwenyezi-Mungu? Mkimwasi Mwenyezi-Mungu leo, kesho ataikasirikia sana jumuiya nzima ya Israeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, sasa ndiyo mnamwacha BWANA? “ ‘Kama mkimwasi BWANA leo, kesho atalikasirikia kusanyiko lote la Israeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, sasa ndiyo mnamwacha bwana? “ ‘Kama mkimwasi bwana leo, kesho atalikasirikia kusanyiko lote la Israeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
hata ikawa hamna budi hivi leo kugeuka na kuacha kumfuata BWANA? Kisha itakuwa, kwa kuwa ninyi mnamwasi BWANA hivi leo, kwamba kesho yeye atakasirika na mkutano wote wa Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa nini, basi, mmeacha kumfuata Mwenyezi-Mungu? Mkimwasi Mwenyezi-Mungu leo, kesho ataikasirikia sana jumuiya nzima ya Israeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nanyi leo hivi mnarudi nyuma na kumwacha Bwana. Kweli ninyi leo hivi mnamkataa Bwana, msimtii, naye kesho ataukasirikia mkutano wote wa Waisiraeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
hata ikawa hamna budi hivi leo kugeuka na kuacha kumwandama BWANA? Kisha itakuwa, kwa kuwa ninyi mwamwasi BWANA hivi leo, kwamba kesho yeye atakasirika na mkutano wote wa Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa nini, basi, mumeacha kumufuata Yawe? Mukimwasi Yawe leo, kesho atakasirikia sana Waisraeli wote pamoja.