Joshua 22:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Haya, ikiwa nchi yenu si najisi, njoni katika nchi ya Mwenyezi-Mungu ambako hema yake iko na kujichukulia sehemu huko pamoja nasi; ila tu msimwasi Mwenyezi-Mungu na kutufanya sisi sote waasi kwa kujijengea nyinyi wenyewe madhabahu isiyo ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ikiwa nchi mnayomiliki imenajisika, vukeni mje katika nchi ya Mwenyezi Mungu, mahali Maskani ya Mwenyezi Mungu ilipo, nanyi mkajitwalie sehemu miongoni mwetu, lakini msije mkaasi dhidi ya Mwenyezi Mungu wala dhidi yetu sisi kwa kujijengea madhabahu, isipokuwa madhabahu ya Mwenyezi Mungu, Mungu wetu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi kwamba hiyo nchi ya milki yenu si tohara, ndipo ninyi vukeni na kuingia nchi ya milki yake Bwana, ambayo maskani ya Bwana inakaa ndani yake, nanyi twaeni milki kati yetu; lakini msimwasi Bwana, wala msituasi sisi, kwa kujijengea madhabahu zaidi ya hiyo madhabahu ya Bwana, Mungu wetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Haya, ikiwa nchi yenu si najisi, njoni katika nchi ya Mwenyezi-Mungu ambako hema yake iko na kujichukulia sehemu huko pamoja nasi; ila tu msimwasi Mwenyezi-Mungu na kutufanya sisi sote waasi kwa kujijengea nyinyi wenyewe madhabahu isiyo ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama nchi mnayomiliki imenajisika, vukeni mje katika nchi ya BWANA, mahali Maskani ya BWANA ilipo, nanyi mkajitwalie sehemu miongoni mwetu, lakini msije mkaasi dhidi ya BWANA wala dhidi yetu sisi kwa kujijengea madhabahu nyingine kwa ajili yenu, zaidi ya madhabahu ya BWANA Mungu wetu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama nchi mnayomiliki imenajisika, vukeni mje katika nchi ya bwana, mahali Maskani ya bwana ilipo, nanyi mkajitwalie sehemu miongoni mwetu, lakini msije mkaasi dhidi ya bwana wala dhidi yetu sisi kwa kujijengea madhabahu, zaidi ya madhabahu ya bwana Mwenyezi Mungu wetu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi ikiwa hiyo nchi yenu ni najisi, vukeni na kuingia katika nchi ya milki yake BWANA, ambamo maskani ya BWANA inakaa ndani yake, nanyi twaeni milki kati yetu; lakini msimwasi BWANA, wala msituasi sisi, kwa kujijengea madhabahu zaidi ya hiyo madhabahu ya BWANA, Mungu wetu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Haya, ikiwa nchi yenu si najisi, njoni katika nchi ya Mwenyezi-Mungu ambako hema yake iko na kujichukulia sehemu huko pamoja nasi; ila tu msimwasi Mwenyezi-Mungu na kutufanya sisi sote waasi kwa kujijengea nyinyi wenyewe madhabahu isiyo ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nchi hii, mliyoichukua, iwe yenu, kama mnaiona kuwa chafu, haya! Itokeni kwenda katika nchi iliyo yake Bwana, Kao lake Bwana linakokaa, mjipatie katikati yetu nchi ya kuwa yenu! Lakini msimkatae Bwana mkiacha kumtii, wala sisi msitukatae mkiacha kututii mkijijengea pa kutambikia pasipokuwa pake Bwana Mungu wetu pa kutambikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi kwamba hiyo nchi ya milki yenu si tohara, ndipo ninyi vukeni na kuingia nchi ya milki yake BWANA, ambayo maskani ya BWANA inakaa ndani yake, nanyi twaeni milki kati yetu; lakini msimwasi BWANA, wala msituasi sisi, kwa kujijengea madhabahu zaidi ya hiyo madhabahu ya BWANA, Mungu wetu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, ikiwa inchi yenu muliorizi ni chafu, mukuje katika inchi ya Yawe ambako hema yake iko na kujitwalia sehemu kule pamoja nasi; lakini tu musimwasi Yawe na kutufanya sisi wote waasi kwa kujijengea ninyi wenyewe mazabahu isiyokuwa ya Yawe, Mungu wetu.