Joshua 22:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Je, Akani mwana wa Zera alipokosa uaminifu katika vitu vitakatifu, ghadhabu haikuangukia jumuiya nzima ya Israeli? Tena Akani hakufa tu yeye peke yake kwa sababu ya uovu wake.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akani mwana wa Zera alipokosa uaminifu kwa vitu vilivyotengwa kwa ajili ya kuangamizwa, je, ghadhabu haikuwapata kusanyiko lote la Israeli? Si yeye pekee aliyekufa kwa ajili ya dhambi yake.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Je! Huyo Akani mwana wa Zera hakukosa katika vile vitu vilivyowekwa wakfu, na hasira ikauangukia mkutano wote wa Israeli? Kisha mtu huyo hakuangamia peke yake katika uovu wake?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Je, Akani mwana wa Zera alipokosa uaminifu katika vitu vitakatifu, ghadhabu haikuangukia jumuiya nzima ya Israeli? Tena Akani hakufa tu yeye peke yake kwa sababu ya uovu wake.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati Akani mwana wa Zera alipokosa uaminifu kwa vitu vilivyowekwa wakfu, je, ghadhabu ya Mungu haikulipata kusanyiko lote la Israeli? Wala hakuwa yeye peke yake aliyekufa kwa ajili ya hiyo dhambi yake.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati Akani mwana wa Zera alipokosa uaminifu kwa vitu vilivyowekwa wakfu, je, ghadhabu haikulipata kusanyiko lote la Israeli? Hakuwa yeye peke yake aliyekufa kwa ajili ya dhambi yake.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Je! Huyo Akani mwana wa Zera hakukosa katika vile vitu vilivyowekwa wakfu, na hasira ikauangukia mkutano wote wa Israeli? Kisha mtu huyo hakuangamia peke yake katika uovu wake?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Je, Akani mwana wa Zera alipokosa uaminifu katika vitu vitakatifu, ghadhabu haikuangukia jumuiya nzima ya Israeli? Tena Akani hakufa tu yeye peke yake kwa sababu ya uovu wake.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akani, mwana wa Zera, alipouvunja ule mwiko wa kuchukua nyara, makali hayakuutokea mkutano wote wa Waisiraeli? Naye yeye hakuangamia peke yake tu kwa ajili ya hizo manza, alizozikora.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Je! Huyo Akani mwana wa Zera hakukosa katika vile vitu vilivyowekwa wakfu, na hasira ikauangukia mkutano wote wa Israeli? Kisha mtu huyo hakuangamia peke yake katika uovu wake?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akana mwana wa Zera alipokosa uaminifu katika vitu vitakatifu, kasirani haikuangukia Waisraeli wote pamoja? Tena Akana hakukufa tu yeye peke yake kwa sababu ya uovu wake.’ ”