Joshua 22:23 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama tumemwacha Mwenyezi-Mungu tukajenga madhabahu yetu wenyewe ili tutoe sadaka za kuteketezwa, za nafaka au za amani, basi Mwenyezi-Mungu na atulipize kisasi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama tumejijengea madhabahu yetu wenyewe ili kumwacha Mwenyezi Mungu, na kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za nafaka, au kutoa sadaka za amani juu yake, Mwenyezi Mungu mwenyewe na atupatilize leo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
sisi kujijengea madhabahu ili kukengeuka na kuacha kumwandama Bwana; au kama ni kusongeza juu yake sadaka ya kuteketezwa, au sadaka ya unga, au kama ni kusongeza sadaka za amani juu yake, yeye Bwana mwenyewe na alitake jambo hili;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama tumemwacha Mwenyezi-Mungu tukajenga madhabahu yetu wenyewe ili tutoe sadaka za kuteketezwa, za nafaka au za amani, basi Mwenyezi-Mungu na atulipize kisasi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama tumejijengea madhabahu yetu wenyewe ili kumwacha BWANA na kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za nafaka, au kutoa sadaka za amani juu yake, BWANA mwenyewe na atupatilize leo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama tumejijengea madhabahu yetu wenyewe ili kumwacha bwana na kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za nafaka, au kutoa sadaka za amani juu yake, bwana mwenyewe na atupatilize leo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kama tumejijengea madhabahu ili kukengeuka na kuacha kumfuata BWANA; au kama ni kusongeza juu yake sadaka ya kuteketezwa, au sadaka ya unga, au kama ni kusongeza sadaka za amani juu yake, yeye BWANA mwenyewe na atulipize kisasi;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama tumemwacha Mwenyezi-Mungu tukajenga madhabahu yetu wenyewe ili tutoe sadaka za kuteketezwa, za nafaka au za amani, basi Mwenyezi-Mungu na atulipize kisasi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama tumejijengea pale pa kutambikia, tupate kurudi nyuma na kumwacha Bwana, au kwa kwamba tupate pa kutolea ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima pamoja na vipaji vya tambiko au pa kuchinjia ng'ombe za shukrani, basi, Bwana mwenyewe na atupatilize!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
sisi kujijengea madhabahu ili kukengeuka na kuacha kumwandama BWANA; au kama ni kusongeza juu yake sadaka ya kuteketezwa, au sadaka ya unga, au kama ni kusongeza sadaka za amani juu yake, yeye BWANA mwenyewe na alitake jambo hili;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama tumemwacha Yawe tukajenga mazabahu yetu wenyewe kusudi tutoe sadaka za kuteketezwa kwa moto, za unga au za amani, basi Yawe atulipize kisasi.