Joshua 22:24 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini sivyo ilivyo. Tuliijenga kwa kuogopa kwamba huenda katika siku zijazo watoto wenu watawaambia watoto wetu, ‘Nyinyi mna uhusiano gani na Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Sivyo! Tulifanya hivyo kwa hofu kwamba siku zijazo wazao wenu wanaweza wakawaambia wazao wetu, ‘Mna uhusiano gani na Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
au kama sisi tumefanya jambo hili kwa hadhari sana, tena makusudi, huku tukisema, Katika siku zijazo wana wenu yamkini wakanena na wana wetu, na kusema, Ninyi mna nini na Bwana, yeye Mungu wa Israeli?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini sivyo ilivyo. Tuliijenga kwa kuogopa kwamba huenda katika siku zijazo watoto wenu watawaambia watoto wetu, ‘Nyinyi mna uhusiano gani na Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Sivyo! Tulifanya hivyo kwa hofu kwamba siku zijazo wazao wenu wanaweza wakawaambia wazao wetu, ‘Mna uhusiano gani na BWANA, Mungu wa Israeli?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Sivyo! Tulifanya hivyo kwa hofu kwamba siku zijazo wazao wenu wanaweza wakawaambia wazao wetu, ‘Mna uhusiano gani na bwana, Mungu wa Israeli?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
au kama sisi tumefanya jambo hili kwa hofu kuwa, katika siku zijazo wana wenu huenda wakanena na wana wetu na kusema, Ninyi mna uhusiano gani na BWANA, Mungu wa Israeli?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini sivyo ilivyo. Tuliijenga kwa kuogopa kwamba huenda katika siku zijazo watoto wenu watawaambia watoto wetu, ‘Nyinyi mna uhusiano gani na Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini hivi sivyo, ila tumevifanya hivi kwa kulihangaikia jambo hili la kwamba: Kesho wana wenu watawaambia wana wetu kwamba: Ninyi mko na bia gani na Bwana Mungu wa Isiraeli?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
au kama sisi tumefanya jambo hili kwa hadhari sana, tena makusudi, huku tukisema, Katika siku zijazo wana wenu yamkini wakanena na wana wetu, na kusema, Ninyi mna nini na BWANA, yeye Mungu wa Israeli?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini sivyo inavyokuwa. Tuliijenga kwa kuogopa kwamba labda katika siku zinazokuja watoto wenu watawaambia watoto wetu: ‘Ninyi muko na uhusiano gani na Yawe, Mungu wa Israeli?