Joshua 22:25 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hamwoni kwamba Mwenyezi-Mungu ameweka mto wa Yordani kuwa mpaka kati yenu na sisi? Nyinyi makabila ya Reubeni na kabila la Gadi hamna fungu lolote lenu kwa Mwenyezi-Mungu.’ Hivyo watoto wenu wangeweza baadaye kusababisha watoto wetu waache kumwabudu Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu ameifanya Yordani kuwa mpaka kati yetu na ninyi, ninyi Wareubeni na Wagadi! Hamna fungu kwa Mwenyezi Mungu.’ Kwa hiyo wazao wenu wanaweza wakawasababisha wazao wetu wakaacha kumcha Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa yeye Bwana ameufanya huu mto wa Yordani uwe mpaka katikati ya sisi na ninyi, enyi wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, hamna fungu katika Bwana; basi hivyo wana wenu wangewakomesha wana wetu wasimche Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hamwoni kwamba Mwenyezi-Mungu ameweka mto wa Yordani kuwa mpaka kati yenu na sisi? Nyinyi makabila ya Reubeni na kabila la Gadi hamna fungu lolote lenu kwa Mwenyezi-Mungu.’ Hivyo watoto wenu wangeweza baadaye kusababisha watoto wetu waache kumwabudu Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA ameifanya Yordani kuwa mpaka kati yetu na ninyi, ninyi Wareubeni na Wagadi! Hamna fungu kwa BWANA.’ Kwa hiyo wazao wenu wanaweza wakawasababisha wazao wetu wakaacha kumcha BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana ameifanya Yordani kuwa mpaka kati yetu na ninyi, ninyi Wareubeni na Wagadi! Hamna fungu kwa bwana.’ Kwa hiyo wazao wenu wanaweza wakawasababisha wazao wetu wakaacha kumcha bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa yeye BWANA ameufanya huu mto wa Yordani uwe mpaka katikati yetu nanyi, enyi wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, hamna fungu katika BWANA; basi hivyo wana wenu wangeweza kuwafanya wana wetu waache kumwabudu BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hamwoni kwamba Mwenyezi-Mungu ameweka mto wa Yordani kuwa mpaka kati yenu na sisi? Nyinyi makabila ya Reubeni na kabila la Gadi hamna fungu lolote lenu kwa Mwenyezi-Mungu.’ Hivyo watoto wenu wangeweza baadaye kusababisha watoto wetu waache kumwabudu Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana aliuweka Yordani kuwa mpaka wa kututenga sisi nanyi, wana wa Rubeni na wana wa Gadi, hakuna fungu lenu lililoko kwa Bwana! Hivyo wana wenu wangewakomesha wana wetu, wasimwogope Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa yeye BWANA ameufanya huu mto wa Yordani uwe mpaka katikati ya sisi na ninyi, enyi wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, hamna fungu katika BWANA; basi hivyo wana wenu wangewakomesha wana wetu wasimche BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hamwoni kwamba Yawe ameweka muto wa Yordani kuwa mupaka kati yenu na sisi? Ninyi makabila ya Rubeni na kabila la Gadi hamuna fungu lolote lenu kwa Yawe.’ Hivyo watoto wenu wangeweza kisha kusababisha watoto wetu waache kumwabudu Yawe.