Joshua 22:27 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
bali tulitaka madhabahu hii iwe ushuhuda kati yetu na nyinyi na vizazi vyetu vijavyo kwamba sisi tunayo haki ya kumtumikia Mwenyezi-Mungu kwa sadaka zetu za kuteketezwa na tambiko zetu, na kwa sadaka zetu za amani, ili watoto wenu wasije wakawaambia watoto wetu kwamba hawana fungu lolote lao kwa Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Badala yake, itakuwa ni ushahidi kati yetu na ninyi na vizazi vijavyo, kwamba tutamwabudu Mwenyezi Mungu katika mahali patakatifu pake pamoja na sadaka zetu za kuteketezwa, dhabihu na sadaka za amani. Ndipo katika siku zijazo, wazao wenu hawataweza kuwaambia wazao wetu, ‘Ninyi hamna fungu katika Mwenyezi Mungu.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
bali itakuwa ni ushahidi kati ya sisi na ninyi, tena kati ya vizazi vyetu baada yetu, ili kwamba tufanye huo utumishi wa Bwana mbele yake kwa njia ya sadaka zetu za kuteketezwa, na kwa dhabihu zetu, na kwa sadaka zetu za amani; ili kwamba wana wenu wasiwaambie wana wetu katika zamani zijazo, Ninyi hamna fungu katika Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
bali tulitaka madhabahu hii iwe ushuhuda kati yetu na nyinyi na vizazi vyetu vijavyo kwamba sisi tunayo haki ya kumtumikia Mwenyezi-Mungu kwa sadaka zetu za kuteketezwa na tambiko zetu, na kwa sadaka zetu za amani, ili watoto wenu wasije wakawaambia watoto wetu kwamba hawana fungu lolote lao kwa Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Badala yake, itakuwa ni ushahidi kati yetu na ninyi na vizazi vijavyo, kwamba tutamwabudu BWANA katika mahali patakatifu pake pamoja na sadaka zetu za kuteketezwa, dhabihu na sadaka za amani. Ndipo siku zijazo wazao wenu hawataweza kuwaambia wazao wetu, ‘Ninyi hamna fungu katika BWANA.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Badala yake, itakuwa ni ushahidi kati yetu na ninyi na vizazi vijavyo, kwamba tutamwabudu bwana katika mahali patakatifu pake pamoja na sadaka zetu za kuteketezwa, dhabihu na sadaka za amani. Ndipo katika siku zijazo, wazao wenu hawataweza kuwaambia wazao wetu, ‘Ninyi hamna fungu katika bwana.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
bali iwe ushahidi kati yetu nanyi, tena kati ya vizazi vyetu baada yetu, kwamba sisi tunamhudumia BWANA kwa njia ya sadaka zetu za kuteketezwa, na kwa dhabihu zetu, na kwa sadaka zetu za amani; ili kwamba wana wenu wasiwaambie wana wetu katika siku zijazo, Ninyi hamna fungu katika BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
bali tulitaka madhabahu hii iwe ushuhuda kati yetu na nyinyi na vizazi vyetu vijavyo kwamba sisi tunayo haki ya kumtumikia Mwenyezi-Mungu kwa sadaka zetu za kuteketezwa na tambiko zetu, na kwa sadaka zetu za amani, ili watoto wenu wasije wakawaambia watoto wetu kwamba hawana fungu lolote lao kwa Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
ila pawe pa kutushuhudia sisi nanyi na vizazi vyetu vitakavyokuwa nyuma yetu, ya kama nasi tunamtumikia Bwana machoni pake na kumtolea ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima na nyingine zinazoteketezwa vipande vipande tu, hata za shukrani, wana wenu wasiwaambie wana wetu kesho: Hakuna fungu lenu lililoko kwa Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
bali itakuwa ni ushahidi kati ya sisi na ninyi, tena kati ya vizazi vyetu baada yetu, ili kwamba tufanye huo utumishi wa BWANA mbele yake kwa njia ya sadaka zetu za kuteketezwa, na kwa dhabihu zetu, na kwa sadaka zetu za amani; ili kwamba wana wenu wasiwaambie wana wetu katika zamani zijazo, Ninyi hamna fungu katika BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
lakini tulitaka mazabahu hii ikuwe ushuhuda kati yetu na ninyi na vizazi vyetu vinavyokuja kwamba sisi tuna haki ya kumutumikia Yawe kwa sadaka zetu za kuteketezwa kwa moto na sadaka zetu zingine, na kwa sadaka zetu za amani, kusudi watoto wenu wasipate kuwaambia watoto wetu kwamba hawana fungu lolote lao kwa Yawe.