Joshua 22:29 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sisi hatukuwa na nia ya kumwasi sasa Mwenyezi-Mungu hata kidogo na kumwacha kwa kujenga madhabahu ya kutolea sadaka za kuteketezwa au sadaka za unga au za tambiko. Hatupendi kutolea sadaka mahali pengine isipokuwa juu ya madhabahu ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu iliyo mbele ya maskani yake.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Hili jambo la kumwasi Mwenyezi Mungu na kumwacha siku hii ya leo kwa kujenga madhabahu kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, sadaka za nafaka na dhabihu, isipokuwa madhabahu ya Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, iliyo mbele ya Maskani yake na liwe mbali nasi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mungu na atuzuie msimwasi Bwana, na kukengeuka hivi leo na kuacha kumwandama Bwana, hata mkajenga madhabahu kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, au sadaka za unga, au dhabihu, mbali na ile madhabahu ya Bwana, Mungu wetu, iliyo huko mbele ya maskani yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sisi hatukuwa na nia ya kumwasi sasa Mwenyezi-Mungu hata kidogo na kumwacha kwa kujenga madhabahu ya kutolea sadaka za kuteketezwa au sadaka za unga au za tambiko. Hatupendi kutolea sadaka mahali pengine isipokuwa juu ya madhabahu ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu iliyo mbele ya maskani yake.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Hili jambo la kumwasi BWANA na kumwacha siku hii ya leo kwa kujenga madhabahu kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, sadaka za nafaka na dhabihu, zaidi ya madhabahu ya BWANA Mungu wetu iliyo mbele ya maskani yake na liwe mbali nasi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Hili jambo la kumwasi bwana na kumwacha siku hii ya leo kwa kujenga madhabahu kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, sadaka za nafaka na dhabihu, zaidi ya madhabahu ya bwana Mwenyezi Mungu wetu iliyo mbele ya maskani yake na liwe mbali nasi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mungu na atuzuie tusimwasi BWANA, na kukengeuka hivi leo na kuacha kumfuata BWANA, hata mkajenga madhabahu kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, au sadaka za unga, au dhabihu, mbali na ile madhabahu ya BWANA, Mungu wetu, iliyo huko mbele ya maskani yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sisi hatukuwa na nia ya kumwasi sasa Mwenyezi-Mungu hata kidogo na kumwacha kwa kujenga madhabahu ya kutolea sadaka za kuteketezwa au sadaka za unga au za tambiko. Hatupendi kutolea sadaka mahali pengine isipokuwa juu ya madhabahu ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu iliyo mbele ya maskani yake.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Na litukalie mbali shauri kama hilo la kumkataa Bwana, tusimtii, nalo la kurudi nyuma sasa na kumwacha Bwana, tukijijengea pa kutambikia, pawe pa kuteketezea ng'ombe nzima za tambiko na pa kutolea vipaji vya tambiko na pa kuchinjia ng'ombe nyingine za tambiko, pasipokuwa pale pa kumtambikia Bwana Mungu wetu palipo mbele ya Kao lake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mungu na atuzuie msimwasi BWANA, na kukengeuka hivi leo na kuacha kumwandama BWANA, hata mkajenga madhabahu kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, au sadaka za unga, au dhabihu, mbali na ile madhabahu ya BWANA, Mungu wetu, iliyo huko mbele ya maskani yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sisi hatukuwa na nia ya kumwasi sasa Yawe hata kidogo na kumwacha kwa kujenga mazabahu ya kutolea sadaka za kuteketezwa kwa moto au sadaka za unga au sadaka zingine. Hatupendi kutolea sadaka pahali pengine isipokuwa juu ya mazabahu ya Yawe, Mungu wetu, inayokuwa katika makao yake.”