Joshua 22:30 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kuhani Finehasi, viongozi wa jumuiya nzima na wakuu wa jamaa za Israeli waliokuwa pamoja naye waliposikia maneno hayo ya watu wa makabila ya Reubeni na Gadi na nusu ya kabila la Manase, wakaridhika.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kuhani Finehasi na viongozi wa kusanyiko, hao wakuu wa koo za Israeli, waliposikia hayo waliyosema Wareubeni, Wagadi na Manase, wakaridhika.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Finehasi kuhani, na wakuu wa mkutano, maana, ni hao waliokuwa vichwa vya maelfu ya Israeli waliokuwa pamoja naye, hapo walipoyasikia hayo maneno waliyoyasema hao wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na wana wa Manase, maneno hayo yaliwaridhia sana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kuhani Finehasi, viongozi wa jumuiya nzima na wakuu wa jamaa za Israeli waliokuwa pamoja naye waliposikia maneno hayo ya watu wa makabila ya Reubeni na Gadi na nusu ya kabila la Manase, wakaridhika.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati kuhani Finehasi na viongozi wa kusanyiko, wakuu wa koo za Israeli, waliposikia hayo waliyosema hao Wareubeni, Wagadi na hiyo nusu ya kabila la Manase, wakaridhika.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati kuhani Finehasi na viongozi wa kusanyiko na wakuu wa koo za Israeli, waliposikia hayo waliyosema Wareubeni, Wagadi na Manase, wakaridhika.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Finehasi kuhani, na wakuu wa mkutano, na hao vichwa vya maelfu ya Israeli waliokuwa pamoja naye, hapo walipoyasikia hayo maneno waliyoyasema hao wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na wana wa Manase, maneno hayo yaliwaridhisha sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kuhani Finehasi, viongozi wa jumuiya nzima na wakuu wa jamaa za Israeli waliokuwa pamoja naye waliposikia maneno hayo ya watu wa makabila ya Reubeni na Gadi na nusu ya kabila la Manase, wakaridhika.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtambikaji Pinehasi na wakuu wa mkutano waliokuwa vichwa vyao maelfu ya Waisiraeli waliokuwa naye walipoyasikia haya maneno, wana wa Rubeni na wana wa Gadi na wana wa Manase waliyoyasema, wakayaona kuwa mema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Finehasi kuhani, na wakuu wa mkutano, maana, ni hao waliokuwa vichwa vya maelfu ya Israeli waliokuwa pamoja naye, hapo walipoyasikia hayo maneno waliyoyasema hao wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na wana wa Manase, maneno hayo yaliwaridhia sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kuhani Finehasi na wakubwa wa jamaa za Waisraeli waliokuwa pamoja naye waliposikia maneno hayo ya watu wa makabila ya Rubeni na Gadi na nusu ya kabila la Manase, wakafurahi.