Joshua 22:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sasa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu amewapa ndugu zenu amani, kama vile alivyoahidi, basi, rudini kwenu katika nchi ambayo mlipewa na Mose mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, iwe mali yenu, yaani ngambo ya mto Yordani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sasa kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, amewapa ndugu zenu pumziko kama alivyoahidi, rudini nyumbani mwenu katika nchi ambayo Musa mtumishi wa Mwenyezi Mungu aliwapa ng’ambo ya Yordani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na sasa yeye Bwana, Mungu wenu, amewapa ndugu zenu kustarehe, kama alivyowaambia; basi sasa rudini ninyi mwende mahemani kwenu, hata nchi ya milki yenu, ambayo huyo Musa, mtumishi wa Bwana, aliwapa ng'ambo ya pili ya Yordani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sasa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu amewapa ndugu zenu amani, kama vile alivyoahidi, basi, rudini kwenu katika nchi ambayo mlipewa na Mose mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, iwe mali yenu, yaani ng'ambo ya mto Yordani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sasa kwa kuwa BWANA Mungu wenu amewapa ndugu zenu raha kama alivyoahidi, rudini nyumbani mwenu katika nchi ile ambayo Mose mtumishi wa BWANA aliwapa ng'ambo ya pili ya Yordani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sasa kwa kuwa bwana Mwenyezi Mungu wenu amewapa ndugu zenu pumziko kama alivyoahidi, rudini nyumbani mwenu katika nchi ile ambayo Musa mtumishi wa bwana aliwapa ng’ambo ya Yordani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na sasa yeye BWANA, Mungu wenu, amewapa ndugu zenu kustarehe, kama alivyowaambia; basi sasa rudini ninyi mwende mahemani kwenu, hata nchi ya milki yenu, ambayo huyo Musa, mtumishi wa BWANA, aliwapa ng'ambo ya pili ya Yordani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sasa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu amewapa ndugu zenu amani, kama vile alivyoahidi, basi, rudini kwenu katika nchi ambayo mlipewa na Mose mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, iwe mali yenu, yaani ngambo ya mto Yordani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa Bwana Mungu wenu amewapatia ndugu zenu kutulia, kama alivyowaambia; kwa hiyo geukeni, mwende zenu mahemani kwenu katika nchi hiyo, mliyoichukua, iwe yenu, Mose, mtumishi wa Bwana, aliyowapa ng'ambo ya huko ya Yordani!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na sasa yeye BWANA, Mungu wenu, amewapa ndugu zenu kustarehe, kama alivyowaambia; basi sasa rudini ninyi mwende mahemani kwenu, hata nchi ya milki yenu, ambayo huyo Musa, mtumishi wa BWANA, aliwapa ng’ambo ya pili ya Yordani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sasa Yawe, Mungu wenu, amewapa wandugu zenu amani, kama vile alivyoahidi, basi, murudie kwenu katika inchi ambayo mulipewa na Musa mutumishi wa Yawe, ikuwe mali yenu, ni kusema ngambo ya muto Yordani.