Joshua 22:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Muwe waangalifu kutii amri na sheria ambazo Mose, mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, aliwaamuru: Kumpenda Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mfuate anachotaka na kushika amri zake; mkae pamoja naye na kumtumikia kwa moyo wote na roho yote.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini mwe waangalifu sana kushika amri na sheria ambazo Musa mtumishi wa Mwenyezi Mungu aliwapa: yaani kumpenda Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, na kuenenda katika njia zake zote, kutii amri zake, kushikamana naye kwa uthabiti na kumtumikia kwa moyo wote na roho yote.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini mjibidiishe sana kuzifanya amri na sheria, ambazo Musa, mtumishi wa Bwana, aliwaamuru, kumpenda Bwana, Mungu wenu, na kwenenda katika njia zake zote, na kuzishika amri zake, na kushikamana na yeye, na kumtumikia kwa moyo wenu wote na nafsi yenu yote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Muwe waangalifu kutii amri na sheria ambazo Mose, mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, aliwaamuru: kumpenda Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mfuate anachotaka na kushika amri zake; mkae pamoja naye na kumtumikia kwa moyo wote na roho yote.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini mwe waangalifu sana kushika amri na sheria zile Mose mtumishi wa BWANA alizowapa: yaani kumpenda BWANA Mungu wenu na kuenenda katika njia zake zote, kutii amri zake, kushikamana naye kwa uthabiti na kumtumikia kwa moyo wenu wote na roho yenu yote.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini mwe waangalifu sana kushika amri na sheria zile Musa mtumishi wa bwana alizowapa: yaani kumpenda bwana Mwenyezi Mungu wenu na kuenenda katika njia zake zote, kutii amri zake, kushikamana naye kwa uthabiti na kumtumikia kwa moyo wenu wote na roho yenu yote.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini mjibidiishe sana kuzifanya amri na sheria, ambazo Musa, mtumishi wa BWANA, aliwaamuru, kumpenda BWANA, Mungu wenu, na kuenenda katika njia zake zote, na kuzishika amri zake, na kushikamana naye, na kumtumikia kwa moyo wenu wote na nafsi yenu yote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Muwe waangalifu kutii amri na sheria ambazo Mose, mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, aliwaamuru: Kumpenda Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mfuate anachotaka na kushika amri zake; mkae pamoja naye na kumtumikia kwa moyo wote na roho yote.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mjiangalie tu kabisa, myafanye maagizo na Maonyo, Mose, mtumishi wa Bwana, aliyowaagiza ninyi! Ni yale ya kumpenda Bwana Mungu wenu, mkiendelea katika njia zake zote, mkiyaangalia maagizo yake na kugandamana naye, tena mkimtumikia kwa mioyo yenu yote na kwa roho zenu zote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini mjibidiishe sana kuzifanya amri na sheria, ambazo Musa, mtumishi wa BWANA, aliwaamuru, kumpenda BWANA, Mungu wenu, na kwenenda katika njia zake zote, na kuzishika amri zake, na kushikamana na yeye, na kumtumikia kwa moyo wenu wote na nafsi yenu yote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mukuwe waangalifu kutii amri na sheria ambazo Musa, mutumishi wa Yawe, aliwaamuru: mumupende Yawe, Mungu wenu, mufuate anachotaka na kushika amri zake, mukae pamoja naye na kumutumikia kwa moyo wote na roho yote.”