Joshua 22:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Rudini makwenu na utajiri mwingi; ng'ombe wenu wote, fedha, dhahabu, shaba, chuma na mavazi mengi. Gawaneni na ndugu zenu nyara zote mlizoziteka kutoka kwa maadui zenu.” Mose alikuwa ameyapa nusu ya kabila la Manase sehemu yao huko Bashani. Naye Yoshua akaipatia nusu ya pili ya kabila hilo sehemu yao huko magharibi ya mto Yordani kama alivyoyapa makabila yale mengine.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
(Kwa nusu ya kabila la Manase, Musa alikuwa amewapa eneo katika Bashani na ile nusu nyingine ya hilo kabila Yoshua aliwapa eneo upande wa magharibi mwa Yordani pamoja na ndugu zao.) Yoshua alipowaaga waende zao nyumbani, aliwabariki,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Musa alikuwa amewapa hiyo nusu moja ya kabila ya Manase urithi katika Bashani; lakini hiyo nusu ya pili Yoshua aliwapa urithi kati ya ndugu zao, ng'ambo ya Yordani upande wa kuelekea magharibi. Zaidi ya hayo Yoshua, hapo alipowapeleka waende zao mahemani kwao, akawabarikia,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Rudini makwenu na utajiri mwingi; ng'ombe wenu wote, fedha, dhahabu, shaba, chuma na mavazi mengi. Gawaneni na ndugu zenu nyara zote mlizoziteka kutoka kwa maadui zenu.” Mose alikuwa ameyapa nusu ya kabila la Manase sehemu yao huko Bashani. Naye Yoshua akaipatia nusu ya pili ya kabila hilo sehemu yao huko magharibi ya mto Yordani kama alivyoyapa makabila yale mengine.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
(Kwa nusu ya kabila la Manase Mose alikuwa amewapa eneo katika Bashani na ile nusu nyingine Yoshua aliwapa eneo upande wa magharibi ya Yordani pamoja na ndugu zao.) Yoshua alipowapeleka waende zao nyumbani mwao, aliwabariki,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
(Kwa nusu ya kabila la Manase Musa alikuwa amewapa eneo katika Bashani na ile nusu nyingine ya hilo kabila Yoshua aliwapa eneo upande wa magharibi ya Yordani pamoja na ndugu zao). Yoshua alipowaaga waende zao nyumbani, aliwabariki,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Musa alikuwa amewapa hiyo nusu moja ya kabila la Manase urithi katika Bashani; lakini hiyo nusu ya pili Yoshua aliwapa urithi kati ya ndugu zao, ng'ambo ya Yordani upande wa kuelekea magharibi. Zaidi ya hayo Yoshua, hapo alipowaruhusu waende zao mahemani kwao, akawabariki,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Rudini makwenu na utajiri mwingi; ng'ombe wenu wote, fedha, dhahabu, shaba, chuma na mavazi mengi. Gawaneni na ndugu zenu nyara zote mlizoziteka kutoka kwa maadui zenu.” Mose alikuwa ameyapa nusu ya kabila la Manase sehemu yao huko Bashani. Naye Yoshua akaipatia nusu ya pili ya kabila hilo sehemu yao huko magharibi ya mto Yordani kama alivyoyapa makabila yale mengine.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nusu ya shina la Manase Mose aliwapa kukaa huko Basani, nayo nusu ya pili Yosua aliwapa kukaa na ndugu zao ng'ambo ya huku ya Yordani inayoelekea baharini; hawa nao Yosua aliwabariki alipowapa ruhusa kwenda mahemani kwao,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Musa alikuwa amewapa hiyo nusu moja ya kabila ya Manase urithi katika Bashani; lakini hiyo nusu ya pili Yoshua aliwapa urithi kati ya ndugu zao, ng’ambo ya Yordani upande wa kuelekea magharibi. Zaidi ya hayo Yoshua, hapo alipowapeleka waende zao mahemani kwao, akawabarikia,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Murudie kwenu na utajiri mwingi; ngombe wenu wote, feza, zahabu, shaba, chuma na nguo nyingi. Mugawanyane na wandugu zenu vitu vyote mulivyonyanganya kutoka kwa waadui zenu.” Musa alikuwa amepatia nusu ya kabila la Manase sehemu yao kule Basani. Naye Yoshua akaipatia nusu ya pili ya kabila lile sehemu yao kule upande wa magaribi wa muto Yordani kama vile alivyoyapatia makabila yale mengine.