Joshua 22:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, watu wa Reubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase wakaachana na watu wa makabila mengine ya Israeli huko Shilo, nchini Kanaani, wakarudi kwao katika nchi ya Gileadi, nchi yao wenyewe waliyoimiliki kwa amri ya Mwenyezi-Mungu kama alivyomwagiza Mose.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase wakawaacha Waisraeli huko Shilo katika nchi ya Kanaani ili kurudi Gileadi, nchi yao wenyewe waliyoipata sawasawa na agizo la Mwenyezi Mungu kupitia Musa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na hiyo nusu ya kabila ya Manase wakarudi, wakatoka kwa wana wa Israeli katika Shilo, ulioko nchi ya Kanaani, ili waende nchi ya Gileadi, hiyo nchi ya milki yao, waliyokuwa wanaimiliki, sawasawa na amri ya Bwana kwa mkono wa Musa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, watu wa Reubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase wakaachana na watu wa makabila mengine ya Israeli huko Shilo, nchini Kanaani, wakarudi kwao katika nchi ya Gileadi, nchi yao wenyewe waliyoimiliki kwa amri ya Mwenyezi-Mungu kama alivyomwagiza Mose.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo Wareubeni, Wagadi na hiyo nusu ya kabila la Manase wakawaacha Waisraeli huko Shilo katika nchi ya Kanaani ili kurudi Gileadi, nchi yao wenyewe waliyoipata sawasawa na agizo la BWANA kupitia Mose.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo Wareubeni, Wagadi na hiyo nusu ya kabila la Manase wakawaacha Waisraeli huko Shilo katika nchi ya Kanaani ili kurudi Gileadi, nchi yao wenyewe waliyoipata sawasawa na agizo la bwana kupitia Musa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na hiyo nusu ya kabila la Manase wakarudi, wakatoka kwa wana wa Israeli katika Shilo, ulioko nchi ya Kanaani, ili waende nchi ya Gileadi, hiyo nchi ya milki yao, waliyokuwa wanaimiliki, sawasawa na amri ya BWANA kwa mkono wa Musa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, watu wa Reubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase wakaachana na watu wa makabila mengine ya Israeli huko Shilo, nchini Kanaani, wakarudi kwao katika nchi ya Gileadi, nchi yao wenyewe waliyoimiliki kwa amri ya Mwenyezi-Mungu kama alivyomwagiza Mose.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Warubeni na Wagadi nao wale wa nusu ya shina la Manase wakarudi na kutoka kwao wana wa Isiraeli kule Silo ulioko katika nchi ya Kanaani, wakashika njia ya kwenda katika nchi ya Gileadi, ndiyo nchi, waliyoichukua, iwe yao, watue huko kwa kuagizwa na Bwana kinywani mwa Mose.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na hiyo nusu ya kabila ya Manase wakarudi, wakatoka kwa wana wa Israeli katika Shilo, ulioko nchi ya Kanaani, ili waende nchi ya Gileadi, hiyo nchi ya milki yao, waliyokuwa wanaimiliki, sawasawa na amri ya BWANA kwa mkono wa Musa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, watu wa Rubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase wakaachana na watu wa makabila mengine ya Israeli kule Shilo katika inchi ya Kanana, wakarudi kwao katika inchi ya Gileadi, inchi yao wenyewe walioirizi kwa amri ya Yawe kama vile alivyomwagiza Musa.