Joshua 23:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini kama vile Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, alivyotimiza mambo yote mema aliyowaahidi, vivyo hivyo anaweza kuwaletea maovu yote mpaka awaangamize nyote kutoka nchi hii nzuri ambayo amewapeni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini kama vile kila ahadi njema ya Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, imekuwa kweli, vivyo hivyo Mwenyezi Mungu ataleta maovu yote kama alivyoonya, hadi awe amewaangamiza kutoka nchi hii nzuri aliyowapa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha itakuwa, kama yalivyowafikilia yale mambo mema yote, Bwana, Mungu wenu, aliyowaahidia ninyi, kadhalika Bwana atawafikilizia mabaya yote, hata atakapokuwa amewaangamiza katika nchi hii njema, Bwana Mungu wenu, aliyowapa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini kama vile Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, alivyotimiza mambo yote mema aliyowaahidi, vivyo hivyo anaweza kuwaletea maovu yote mpaka awaangamize nyote kutoka nchi hii nzuri ambayo amewapeni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Bali kama vile ambavyo kila ahadi njema ya BWANA Mungu wenu imekuwa kweli, vivyo hivyo BWANA ataleta maovu yote aliyosema, mpaka awe amewaangamiza kutoka katika nchi hii nzuri aliyowapa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini kama vile kila ahadi njema ya bwana Mwenyezi Mungu wenu imekuwa kweli, vivyo hivyo bwana ataleta maovu yote kama alivyo onya, mpaka awe amewaangamiza kutoka nchi hii nzuri aliyowapa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha itakuwa, kama yalivyowafikia yale mambo mema yote, BWANA, Mungu wenu, aliyowaahidia ninyi, kadhalika BWANA atawafikilizia mabaya yote, hata atakapokuwa amewaangamiza katika nchi hii njema, BWANA Mungu wenu, aliyowapa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini kama vile Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, alivyotimiza mambo yote mema aliyowaahidi, vivyo hivyo anaweza kuwaletea maovu yote mpaka awaangamize nyote kutoka nchi hii nzuri ambayo amewapeni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini kama yale mema yote, Bwana Mungu wenu aliyowaagia, yalivyowatimilia, vivyo hivyo Bwana atawatimizia nayo yale mabaya yote, mpaka awatoweshe katika nchi hii nzuri, Bwana Mungu wenu aliyowapa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha itakuwa, kama yalivyowafikilia yale mambo mema yote, BWANA, Mungu wenu, aliyowaahidia ninyi, kadhalika BWANA atawafikilizia mabaya yote, hata atakapokuwa amewaangamiza katika nchi hii njema, BWANA Mungu wenu, aliyowapa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kama vile Yawe, Mungu wenu, alivyotimiza mambo yote mema aliyowaahidi, ni vile vile anavyoweza kuwaletea maovu yote mpaka awaangamize wote kutoka inchi hii nzuri ambayo amewapa.