Joshua 23:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama mkivunja agano lake Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, ambalo aliwaamuru mlishike, mkaenda kuitumikia miungu mingine na kuisujudia, basi, hasira ya Mwenyezi-Mungu itawaka juu yenu, nanyi mtaangamia mara moja kutoka nchi hii nzuri ambayo amewapeni.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mkilivunja agano la Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, ambalo aliwaamuru ninyi, mkaenda na kuitumikia miungu mingine na kuisujudia, hasira ya Mwenyezi Mungu itawaka dhidi yenu, basi nanyi mtaangamia kutoka nchi nzuri aliyowapa ninyi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hapo mtakapolivunja agano la Bwana, Mungu wenu, alilowaamuru, na kwenda kuitumikia miungu mingine, na kujiinamisha mbele yao, ndipo hasira ya Bwana itakapowaka juu yenu, nanyi mtaangamia upesi katika nchi hii njema aliyowapa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama mkivunja agano lake Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, ambalo aliwaamuru mlishike, mkaenda kuitumikia miungu mingine na kuisujudia, basi, hasira ya Mwenyezi-Mungu itawaka juu yenu, nanyi mtaangamia mara moja kutoka nchi hii nzuri ambayo amewapeni.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama mkilivunja Agano la BWANA Mungu wenu, ambalo aliwaamuru ninyi, mkaenda na kuitumikia miungu mingine na kuisujudia, hasira ya BWANA itawaka dhidi yenu, nanyi mtaangamia mara kutoka katika nchi nzuri aliyowapa ninyi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama mkilivunja agano la bwana Mwenyezi Mungu wenu, ambalo aliwaamuru ninyi, mkaenda na kuitumikia miungu mingine na kuisujudia, hasira ya bwana itawaka dhidi yenu, nanyi mtaangamia kutoka nchi nzuri aliyowapa ninyi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hapo mtakapolivunja agano la BWANA, Mungu wenu, alilowaamuru, na kwenda kuitumikia miungu mingine, na kujiinamisha mbele yao, ndipo hasira ya BWANA itakapowaka juu yenu, nanyi mtaangamia upesi katika nchi hii njema aliyowapa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama mkivunja agano lake Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, ambalo aliwaamuru mlishike, mkaenda kuitumikia miungu mingine na kuisujudia, basi, hasira ya Mwenyezi-Mungu itawaka juu yenu, nanyi mtaangamia mara moja kutoka nchi hii nzuri ambayo amewapeni.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hayo yatafanyika, msipolishika Agano, Bwana Mungu wenu alilowaagiza, mtakapokwenda kutumikia miungu mingine na kuiangukia, basi, hapo ndipo, makali ya Bwana yatakapowawakia, mwangamie upesi na kutoweka katika nchi hii nzuri, aliyowapa ninyi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hapo mtakapolivunja agano la BWANA, Mungu wenu, alilowaamuru, na kwenda kuitumikia miungu mingine, na kujiinamisha mbele yao, ndipo hasira ya BWANA itakapowaka juu yenu, nanyi mtaangamia upesi katika nchi hii njema aliyowapa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama mukivunja agano la Yawe, Mungu wenu, ambalo aliwaamuru mulishike, mukienda kuitumikia miungu mingine na kuinama mbele yao; basi, hasira ya Yawe itawaka juu yenu, nanyi mutaangamia mara moja kutoka inchi hii nzuri ambayo amewapa.”