Joshua 23:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nchi za mataifa yaliyobaki na yale niliyoyaangamiza nimewagawieni ziwe mali ya makabila yenu, kutoka Yordani mpaka bahari ya Mediteranea, upande wa magharibi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kumbukeni jinsi nilivyowagawia kama urithi kwa makabila yenu yote nchi ya mataifa yaliyobaki, yaani mataifa niliyowashinda, kati ya Mto Yordani na Bahari kuu upande wa magharibi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tazama, nimewagawieni kwa kura mataifa haya yaliyobaki, yawe urithi kwa kabila zenu, toka mto wa Yordani, pamoja na mataifa yote niliyowakatilia mbali, mpaka bahari kubwa upande wa machweo ya jua.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nchi za mataifa yaliyobaki na yale niliyoyaangamiza nimewagawieni ziwe mali ya makabila yenu, kutoka Yordani mpaka bahari ya Mediteranea, upande wa magharibi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kumbukeni jinsi nilivyowagawia kama urithi kwa ajili ya makabila yenu yote nchi ya mataifa yaliyobaki, yaani mataifa niliyowashinda, kati ya Mto Yordani na Bahari ile kuu upande wa magharibi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kumbukeni jinsi nilivyowagawia kama urithi kwa makabila yenu yote nchi ya mataifa yaliyobaki, yaani mataifa niliyowashinda, kati ya Mto Yordani na Bahari kuu upande wa magharibi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tazama, nimewagawieni kwa kura mataifa haya yaliyobaki, yawe urithi kwa makabila yenu, toka mto wa Yordani, pamoja na mataifa yote niliyowakatilia mbali, mpaka bahari kubwa upande wa magharibi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nchi za mataifa yaliyobaki na yale niliyoyaangamiza nimewagawieni ziwe mali ya makabila yenu, kutoka Yordani mpaka bahari ya Mediteranea, upande wa magharibi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tazameni: Nimewagawia nazo nchi zao hao wamizimu waliosalia na kuyapigia mashina yenu kura, wazipate kuwa zao toka mto wa Yordani pamoja nazo za wale wamizimu, niliokwisha kuwatowesha mpaka kwenye Bahari Kubwa, jua linakoingia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tazama, nimewagawieni kwa kura mataifa haya yaliyobaki, yawe urithi kwa kabila zenu, toka mto wa Yordani, pamoja na mataifa yote niliyowakatilia mbali, mpaka bahari kubwa upande wa machweo ya jua.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Inchi za mataifa yaliyobaki na yale niliyoyaangamiza nimewagawanyia zikuwe mali ya makabila yenu, kutoka Yordani mpaka bahari ya Mediteranea, upande wa magaribi.