Joshua 24:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Sasa, basi, mcheni Mwenyezi-Mungu na kumtumikia kwa moyo mnyofu na uaminifu. Acheni kabisa miungu ile ambayo wazee wenu waliiabudu ngambo ya mto Eufrate na nchini Misri. Mtumikieni Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Sasa basi mcheni Mwenyezi Mungu na kumtumikia kwa uaminifu wote. Itupeni mbali miungu ambayo baba zenu waliiabudu huko ng’ambo ya Mto na huko Misri, nanyi mtumikieni Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi sasa mcheni Bwana, mkamtumikie kwa unyofu wa moyo na kwa kweli; na kuiweka mbali miungu ambayo baba zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, na huko Misri; mkamtumikie yeye Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Sasa, basi, mcheni Mwenyezi-Mungu na kumtumikia kwa moyo mnyofu na uaminifu. Acheni kabisa miungu ile ambayo wazee wenu waliiabudu ng'ambo ya mto Eufrate na nchini Misri. Mtumikieni Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Sasa basi mcheni BWANA na kumtumikia kwa uaminifu wote. Itupeni mbali miungu ambayo baba zenu waliiabudu huko ng'ambo ya Mto Eufrati na huko Misri, nanyi mtumikieni BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Sasa basi mcheni bwana na kumtumikia kwa uaminifu wote. Itupeni mbali miungu ambayo baba zenu waliiabudu huko ng’ambo ya Mto Frati na huko Misri, nanyi mtumikieni bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi sasa mcheni BWANA, mkamtumikie kwa unyofu wa moyo na kwa kweli; na kuiweka mbali miungu ambayo baba zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, na huko Misri; mkamtumikie yeye BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Sasa, basi, mcheni Mwenyezi-Mungu na kumtumikia kwa moyo mnyofu na uaminifu. Acheni kabisa miungu ile ambayo wazee wenu waliiabudu ngambo ya mto Eufrate na nchini Misri. Mtumikieni Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa mwogopeni Bwana na kumtumikia kwa mioyo yote na kwa welekevu, mkiiacha miungu, baba zenu waliyoitumikia ng'ambo ya huko ya lile jito kubwa nako kule Misri, mpate kumtumikia Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi sasa mcheni BWANA, mkamtumikie kwa unyofu wa moyo na kwa kweli; na kuiweka mbali miungu ambayo baba zenu waliitumikia ng’ambo ya Mto, na huko Misri; mkamtumikie yeye BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Sasa, basi, mumutii Yawe na kumutumikia kwa moyo wa haki na uaminifu. Muache kabisa miungu ile ambayo wazee wenu waliiabudu ngambo ya muto Furati na katika inchi ya Misri. Mumutumikie Yawe.