Joshua 24:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yoshua akawaambia watu wote, “Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, asema hivi: Hapo zamani, wazee wenu waliishi ngambo ya mto Eufrate, wakaitumikia miungu mingine. Mzee mmoja alikuwa Tera, baba yao Abrahamu na Nahori.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yoshua akawaambia watu wote, “Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, asemalo: ‘Hapo zamani baba zenu, pamoja na Tera baba yake Ibrahimu na Nahori, waliishi ng’ambo ya Mto, nao waliiabudu miungu mingine.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yoshua akawaambia watu wote, Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Baba zenu hapo zamani walikaa ng'ambo ya Mto, maana Tera, baba yake Ibrahimu, naye ni baba yake Nahori; wakaitumikia miungu mingine.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yoshua akawaambia watu wote, “Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, asema hivi: Hapo zamani, wazee wenu waliishi ng'ambo ya mto Eufrate, wakaitumikia miungu mingine. Mzee mmoja alikuwa Tera, baba yao Abrahamu na Nahori.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yoshua akawaambia watu wote, “Hili ndilo BWANA, Mungu wa Israeli, asemalo: ‘Hapo zamani baba zenu, pamoja na Tera baba yake Abrahamu na Nahori, waliishi ng'ambo ya Mto Eufrati nao waliiabudu miungu mingine.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yoshua akawaambia watu wote, “Hili ndilo bwana, Mungu wa Israeli, asemalo: ‘Hapo zamani baba zenu, pamoja na Tera baba yake Ibrahimu na Nahori, waliishi ng’ambo ya Mto nao waliiabudu miungu mingine.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yoshua akawaambia watu wote, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Baba zenu hapo zamani walikaa ng'ambo ya Mto, maana Tera, baba yake Abrahamu na Nahori; waliitumikia miungu mingine.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yoshua akawaambia watu wote, “Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, asema hivi: Hapo zamani, wazee wenu waliishi ngambo ya mto Eufrate, wakaitumikia miungu mingine. Mzee mmoja alikuwa Tera, baba yao Abrahamu na Nahori.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Yosua alipowaambia watu wote: Hivi ndivyo, Bwana Mungu wenu anavyosema: Tangu kale baba zenu, walipokaa ng'ambo ya huko ya lile jito kubwa, naye Tera, babake Aburahamu na babake Nahori, walitumikia miungu mingine.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yoshua akawaambia watu wote, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Baba zenu hapo zamani walikaa ng’ambo ya Mto, maana Tera, baba yake Ibrahimu, naye ni baba yake Nahori; wakaitumikia miungu mingine.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yoshua akawaambia watu wote: “Yawe, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Hapo zamani, wazee wenu waliishi ngambo ya muto Furati, wakaitumikia miungu mingine. Muzee mumoja aliitwa Tera, baba ya Abrahamu na Nahori.