Joshua 24:27 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Halafu akawaambia watu wote, “Jiwe hili ndilo litakalokuwa shahidi kwetu, maana limesikia maneno yote ambayo Mwenyezi-Mungu ametuambia. Kwa hiyo, litashuhudia dhidi yenu, ili msije mkamkana Mungu wenu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yoshua akawaambia watu wote, “Tazameni! Jiwe hili litakuwa shahidi juu yetu. Limesikia maneno yote Mwenyezi Mungu aliyotuambia. Litakuwa shahidi juu yenu kama mtakuwa waongo kwa Mungu wenu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yoshua akawaambia watu wote, Tazama, jiwe hili litakuwa shahidi juu yetu; kwa maana limesikia maneno yote ya Bwana aliyotuambia, basi litakuwa shahidi juu yenu, msije mkamkana Mungu wenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Halafu akawaambia watu wote, “Jiwe hili ndilo litakalokuwa shahidi kwetu, maana limesikia maneno yote ambayo Mwenyezi-Mungu ametuambia. Kwa hiyo, litashuhudia dhidi yenu, ili msije mkamkana Mungu wenu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akawaambia watu wote, “Angalieni! Jiwe hili litakuwa shahidi juu yetu. Limesikia maneno yote BWANA aliyotuambia. Litakuwa shahidi juu yenu kama mtakuwa waongo kwa Mungu wenu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yoshua akawaambia watu wote, “Angalieni! Jiwe hili litakuwa shahidi juu yetu. Limesikia maneno yote bwana aliyotuambia. Litakuwa shahidi juu yenu kama mtakuwa waongo kwa Mungu wenu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yoshua akawaambia watu wote, Tazameni, jiwe hili litakuwa shahidi juu yetu; kwa maana limesikia maneno yote ya BWANA aliyotuambia, basi litakuwa shahidi juu yenu, msije mkamkana Mungu wenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Halafu akawaambia watu wote, “Jiwe hili ndilo litakalokuwa shahidi kwetu, maana limesikia maneno yote ambayo Mwenyezi-Mungu ametuambia. Kwa hiyo, litashuhudia dhidi yenu, ili msije mkamkana Mungu wenu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Yosua akawaambia watu wote: Tazameni! Jiwe hili na lituwie shahidi! Kwani limeyasikia maaneno yote, Bwana aliyoyasema na sisi. Kwa hiyo litakuwa shahidi lenu, msimwongopee Mungu wenu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yoshua akawaambia watu wote, Tazama, jiwe hili litakuwa shahidi juu yetu; kwa maana limesikia maneno yote ya BWANA aliyotuambia, basi litakuwa shahidi juu yenu, msije mkamkana Mungu wenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu akawaambia watu wote: “Jiwe hili ndilo litakalokuwa ushuhuda kwetu, maana limesikia maneno yote ambayo Yawe ametuambia. Kwa hiyo, litashuhudia juu yenu, kusudi musipate kumwasi Mungu wenu.”