Joshua 24:31 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waisraeli walimtumikia Mwenyezi-Mungu muda wote wa uhai wa Yoshua, na baada ya kifo chake, waliendelea kumtumikia kwa muda walioishi wale wazee waliokuwa wameona kwa macho yao mambo yale Mwenyezi-Mungu aliyowatendea Waisraeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Israeli wakamtumikia Mwenyezi Mungu siku zote za maisha ya Yoshua, na za hao wazee walioishi baada ya Yoshua kufa, ambao waliona kila kitu Mwenyezi Mungu alichowatendea Israeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao Israeli wakamtumikia Bwana siku zote za Yoshua, na siku zote za hao wazee walioishi baada ya kufa kwake Yoshua, hao walioijua kazi yote ya Bwana, aliyowatendea Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waisraeli walimtumikia Mwenyezi-Mungu muda wote wa uhai wa Yoshua, na baada ya kifo chake, waliendelea kumtumikia kwa muda walioishi wale wazee waliokuwa wameona kwa macho yao mambo yale Mwenyezi-Mungu aliyowatendea Waisraeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Israeli wakamtumikia BWANA wakati wote wa kipindi cha Yoshua, na kipindi cha hao wazee walioishi baada ya Yoshua kufa na ambao waliona wenyewe kila kitu BWANA alichowatendea Israeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Israeli wakamtumikia bwana siku zote za maisha ya Yoshua, na za hao wazee walioishi baada ya Yoshua kufa, ambao waliona kila kitu bwana alichowatendea Israeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao Israeli wakamtumikia BWANA siku zote za Yoshua, na siku zote za hao wazee walioishi baada ya kufa kwake Yoshua, hao walioijua kazi yote ya BWANA, aliyowatendea Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waisraeli walimtumikia Mwenyezi-Mungu muda wote wa uhai wa Yoshua, na baada ya kifo chake, waliendelea kumtumikia kwa muda walioishi wale wazee waliokuwa wameona kwa macho yao mambo yale Mwenyezi-Mungu aliyowatendea Waisraeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao Waisiraeli wakamtumikia Bwana siku zote, Yosua alizokuwapo, nazo siku zote, walizokuwapo wale wazee waliokaa siku nyingi kuliko Yosua, ndio wale walioyajua yale matendo yote, Bwana aliyowatendea Waisiraeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao Israeli wakamtumikia BWANA siku zote za Yoshua, na siku zote za hao wazee walioishi baada ya kufa kwake Yoshua, hao walioijua kazi yote ya BWANA, aliyowatendea Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waisraeli walimutumikia Yawe muda wote wa maisha ya Yoshua, na nyuma ya kifo chake, waliendelea kumutumikia kwa muda wa maisha ya wale wazee waliokuwa wameona kwa macho yao mambo yale Yawe aliyowatendea Waisraeli.