Joshua 24:33 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye Eleazari, mwana wa Aroni, akafariki na kuzikwa Gibea, mji ambao alikuwa amepewa mwanawe Finehasi katika nchi ya milima ya Efraimu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Naye Eleazari mwana wa Haruni akafariki, akazikwa huko Gibea, mlima aliokuwa amepewa mtoto wake Finehasi, kwenye nchi ya vilima ya Efraimu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Huyo Eleazari mwana wa Haruni naye akafa; wakamzika katika kilima cha Finehasi mwanawe, ambacho alipewa yeye katika nchi ya vilima ya Efraimu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye Eleazari, mwana wa Aroni, akafariki na kuzikwa Gibea, mji ambao alikuwa amepewa mwanawe Finehasi katika nchi ya milima ya Efraimu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Naye Eleazari mwana wa Aroni akafariki akazikwa huko Gibeathi, ambapo alikuwa amepewa mtoto wake Finehasi, kwenye nchi ya vilima ya Efraimu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Naye Eleazari mwana wa Haruni akafariki akazikwa huko Gibea, mlima aliokuwa amepewa mtoto wake Finehasi, kwenye nchi ya vilima ya Efraimu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Huyo Eleazari mwana wa Haruni naye akafa; wakamzika Gibea, mji wa Finehasi mwanawe, ambao alipewa katika nchi ya vilima ya Efraimu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye Eleazari, mwana wa Aroni, akafariki na kuzikwa Gibea, mji ambao alikuwa amepewa mwanawe Finehasi katika nchi ya milima ya Efraimu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Elazari, mwana wa Haroni, alipokufa, wakamzika huko Gibea uliokuwa mji wa mwanawe Pinehasi, maana ndio, aliogawiwa milimani kwa Efuraimu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Huyo Eleazari mwana wa Haruni naye akafa; wakamzika katika kilima cha Finehasi mwanawe, ambacho alipewa yeye katika nchi ya vilima ya Efraimu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye Eleazari mwana wa Haruni, akakufa na kuzikwa Gibea, muji ambao mwana wake Finehasi alikuwa amepewa katika inchi ya milima ya Efuraimu.