Joshua 24:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waisraeli waliponililia mimi Mwenyezi-Mungu, niliweka giza kati yao na Wamisri na kuifanya bahari iwafunike Wamisri. Nyinyi wenyewe mlijionea yale niliyowatendea Wamisri. Mliishi jangwani muda mrefu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini wakamlilia Mwenyezi Mungu wakitaka msaada, naye akaweka giza kati yenu na Wamisri, akaileta bahari juu yao ikawafunika. Ninyi mliona kwa macho yenu wenyewe kile nilichowatendea Wamisri. Kisha mliishi jangwani kwa muda mrefu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao walipomlilia Bwana, akaweka giza kati ya ninyi na Wamisri, akaileta bahari juu yao, akawafunikiza; nayo macho yenu yaliyaona mambo niliyoyatenda huko Misri; kisha mkakaa jangwani siku nyingi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waisraeli waliponililia mimi Mwenyezi-Mungu, niliweka giza kati yao na Wamisri na kuifanya bahari iwafunike Wamisri. Nyinyi wenyewe mlijionea yale niliyowatendea Wamisri. Mliishi jangwani muda mrefu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini wakamlilia BWANA wakitaka msaada, Mungu akaweka giza kati yenu na Wamisri, akaileta bahari juu yao ikawafunika. Ninyi mliona kwa macho yenu wenyewe kile nilichowatendea Wamisri. Kisha mliishi jangwani kwa muda mrefu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini wakamlilia bwana wakitaka msaada, naye akaweka giza kati yenu na Wamisri, akaileta bahari juu yao ikawafunika. Ninyi mliona kwa macho yenu wenyewe kile nilichowatendea Wamisri. Kisha mliishi jangwani kwa muda mrefu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao walipomlilia BWANA, akaweka giza kati yenu na Wamisri, akaileta bahari juu yao, akawafunikiza; nayo macho yenu yaliyaona mambo niliyoyatenda huko Misri; kisha mkakaa jangwani siku nyingi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waisraeli waliponililia mimi Mwenyezi-Mungu, niliweka giza kati yao na Wamisri na kuifanya bahari iwafunike Wamisri. Nyinyi wenyewe mlijionea yale niliyowatendea Wamisri. Mliishi jangwani muda mrefu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walipomlilia Bwana, akaangusha giza jeusi, liwe katikati yenu na Wamisri; halafu akaleta bahari, iwatose na kuwafunika. Macho yenu yaliyaona hayo, niliyowafanyizia Wamisri, kisha mkakaa nyikani siku nyingi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao walipomlilia BWANA, akaweka giza kati ya ninyi na Wamisri, akaileta bahari juu yao, akawafunikiza; nayo macho yenu yaliyaona mambo niliyoyatenda huko Misri; kisha mkakaa jangwani siku nyingi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waisraeli waliponililia mimi Yawe, niliweka giza kati yao na Wamisri na kuifanya bahari iwafunike Wamisri. Ninyi wenyewe mulijionea yale niliyowatendea Wamisri. Muliishi katika jangwa muda murefu.