Joshua 3:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati nyayo za makuhani wanaobeba sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu, Bwana wa dunia yote, zitakapoingia katika maji ya mto Yordani, maji ya mto huo yataacha kutiririka. Na yale yatakayokuwa yanatiririka kutoka upande wa juu yatajikusanya pamoja kama rundo.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mara tu nyayo za makuhani walichukualo Sanduku la Mwenyezi Mungu, Bwana wa dunia yote, zitakapokanyaga ndani ya Mto Yordani, maji hayo yanayotiririka kutoka juu yatatindika na kusimama kama chuguu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Itakuwa, wakati nyayo za makuhani walichukuao sanduku la Bwana, Bwana wa dunia yote, zitakaposimama katika maji ya Yordani, hayo maji ya Yordani yatatindika, maji yale yashukayo kutoka juu; nayo yatasimama kama chuguu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati nyayo za makuhani wanaobeba sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu, Bwana wa dunia yote, zitakapoingia katika maji ya mto Yordani, maji ya mto huo yataacha kutiririka. Na yale yatakayokuwa yanatiririka kutoka upande wa juu yatajikusanya pamoja kama rundo.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mara tu nyayo za makuhani walichukualo Sanduku la BWANA, Bwana wa dunia yote, zitakapokanyaga ndani ya Mto Yordani, maji hayo yatiririkayo kutoka juu yatatindika na kusimama kama chuguu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mara tu nyayo za makuhani walichukualo Sanduku la bwana, Bwana wa dunia yote, zitakapokanyaga ndani ya Mto Yordani, maji hayo yatiririkayo kutoka juu yatatindika na kusimama kama chuguu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Itakuwa, wakati nyayo za makuhani walichukuao sanduku la BWANA, Bwana wa dunia yote, zitakaposimama katika maji ya Yordani, hayo maji ya Yordani yataacha kutiririka, maji yale yashukayo kutoka juu; nayo yatasimama kama kichuguu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati nyayo za makuhani wanaobeba sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu, Bwana wa dunia yote, zitakapoingia katika maji ya mto Yordani, maji ya mto huo yataacha kutiririka. Na yale yatakayokuwa yanatiririka kutoka upande wa juu yatajikusanya pamoja kama rundo.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Itakuwa hapo, nyayo za miguu ya watambikaji wanaolichukua Sanduku la Agano la Bwana wa nchi zote zitakapoyagusa maji ya Yordani, ndipo, maji ya Yordai yatakapojitenga, hayo maji yanayoshuka nayo yanayotoka juu, haya yasimame kuwa kama boma moja tu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Itakuwa, wakati nyayo za makuhani walichukuao sanduku la BWANA, Bwana wa dunia yote, zitakaposimama katika maji ya Yordani, hayo maji ya Yordani yatatindika, maji yale yashukayo kutoka juu; nayo yatasimama kama chuguu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati miguu ya makuhani wanaobeba Sanduku la Agano la Yawe, Bwana wa dunia yote, itakapoingia katika maji ya muto Yordani, maji ya muto huo yataacha kutiririka. Na yale yatakayokuwa yanatiririka kutoka upande wa juu yatajikusanya pamoja kama lundo.”