Joshua 3:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
maji yaliyokuwa yanatiririka kutoka upande wa juu yalisimama na kurundikana mpaka huko Adamu kijiji kilicho karibu na mji wa Sarethani. Maji yaliyokuwa yanateremka kwenda bahari ya Araba, yaani Bahari ya Chumvi, yalitoweka kabisa, watu wakavuka mbele ya Yeriko.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
maji hayo yaliyotiririka kutoka upande wa juu yaliacha kutiririka yakasimama kama chuguu mbali kabisa nao, kwenye mji ulioitwa Adamu kwenye eneo la Sarethani, wakati yale maji yaliyokuwa yanatiririka kuingia kwenye Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi), yalitindika kabisa. Hivyo watu wakavuka kukabili Yeriko.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ndipo hayo maji yaliyoshuka kutoka juu yakasimama, yakainuka, yakawa chuguu, mbali sana, huko Adamu, mji ule ulio karibu na Sarethani, na maji yale yaliyotelemkia bahari ya Araba, yaani Bahari ya Chumvi, yakatindika kabisa; watu wakavuka kukabili Yeriko.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
maji yaliyokuwa yanatiririka kutoka upande wa juu yalisimama na kurundikana mpaka huko Adamu kijiji kilicho karibu na mji wa Sarethani. Maji yaliyokuwa yanateremka kwenda bahari ya Araba, yaani Bahari ya Chumvi, yalitoweka kabisa, watu wakavuka mbele ya Yeriko.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
maji hayo yaliyotiririka kutoka upande wa juu yalitindika yakasimama kama chuguu mbali nao, kwenye mji ulioitwa Adamu karibu na Sarethani, wakati yale maji yaliyokuwa yanatiririka kuingia kwenye Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi), yalikauka kabisa. Hivyo watu wakavuka kukabili Yeriko.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
maji hayo yaliyotiririka kutoka upande wa juu yaliacha kutiririka yakasimama kama chuguu mbali kabisa nao, kwenye mji ulioitwa Adamu kwenye eneo la Sarethani, wakati yale maji yaliyokuwa yanatiririka kuingia kwenye Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi), yalitindika kabisa. Hivyo watu wakavuka kukabili Yeriko.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ndipo hayo maji yaliyoshuka kutoka juu yakasimama, yakainuka, yakawa kichuguu, mbali sana, huko Adamu, mji ule ulio karibu na Sarethani, na maji yale yaliyoteremkia bahari ya Araba, yaani Bahari ya Chumvi, yakaacha kutiririka kabisa; watu wakavuka kukabili Yeriko.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
maji yaliyokuwa yanatiririka kutoka upande wa juu yalisimama na kurundikana mpaka huko Adamu kijiji kilicho karibu na mji wa Sarethani. Maji yaliyokuwa yanateremka kwenda bahari ya Araba, yaani Bahari ya Chumvi, yalitoweka kabisa, watu wakavuka mbele ya Yeriko.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
ndipo, maji yaliyotoka upande wa juu yaliposimama, yakafurika juu kuwa kama boma moja tu, yakafika mbali sana mpaka mji wa Adamu ulioko upande wa Sartani; nayo maji yaliyoshuka kuingia katika bahari ya nyikani, ile Bahari ya Chumvi, yakapwa yote pia; kwa hiyo watu wakapata kuvuka na kuuelekea mji wa Yeriko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ndipo hayo maji yaliyoshuka kutoka juu yakasimama, yakainuka, yakawa chuguu, mbali sana, huko Adamu, mji ule ulio karibu na Sarethani, na maji yale yaliyotelemkia bahari ya Araba, yaani Bahari ya Chumvi, yakatindika kabisa; watu wakavuka kukabili Yeriko.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
maji yaliyokuwa yanatiririka kutoka upande wa juu yalisimama na kulundikana mpaka kule Adamu kijiji kinachokuwa karibu na muji wa Zaretani. Maji yaliyokuwa yanateremuka kwenda katika bahari ya Araba, ni kusema bahari ya Chumvi, yalitoweka kabisa, watu wakavuka mbele ya Yeriko.