Joshua 4:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wale makuhani waliobeba sanduku la agano, walisimama katikati ya mto Yordani mpaka watu walipomaliza kutekeleza kila kitu ambacho Mwenyezi-Mungu alimwamuru Yoshua awaambie watu; Yoshua alifanya yote ambayo Mose alikuwa amemwamuru. Watu wakaharakisha kuvuka mto,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Makuhani waliobeba lile Sanduku walibakia wakiwa wamesimama katikati ya Mto Yordani hadi kila kitu Mwenyezi Mungu alichomwamuru Yoshua kilipokuwa kimekamilishwa na watu, sawasawa na vile Musa alivyokuwa amemwamuru Yoshua. Watu wakafanya haraka kuvuka,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa makuhani waliolichukua hilo sanduku walisimama katikati ya Yordani, hata mambo yote Bwana aliyomwamuru Yoshua awambie hao watu yakaisha, sawasawa na hayo yote Musa aliyokuwa amemwamuru Yoshua; kisha hao watu wakafanya haraka wakavuka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wale makuhani waliobeba sanduku la agano, walisimama katikati ya mto Yordani mpaka watu walipomaliza kutekeleza kila kitu ambacho Mwenyezi-Mungu alimwamuru Yoshua awaambie watu; Yoshua alifanya yote ambayo Mose alikuwa amemwamuru. Watu wakaharakisha kuvuka mto,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Makuhani waliobeba lile Sanduku walibakia wakiwa wamesimama katikati ya Mto Yordani mpaka kila kitu BWANA alichomwamuru Yoshua kilipokuwa kimefanywa na watu, sawasawa na vile Mose alivyokuwa amemwamuru Yoshua! Watu wakafanya haraka kuvuka,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Makuhani waliobeba lile Sanduku walibakia wakiwa wamesimama katikati ya Mto Yordani mpaka kila kitu bwana alichomwamuru Yoshua kilipokuwa kimefanywa na watu, sawasawa na vile Musa alivyokuwa amemwamuru Yoshua. Watu wakafanya haraka kuvuka,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa makuhani waliolichukua hilo sanduku walisimama katikati ya Yordani, hadi mambo yote BWANA aliyomwamuru Yoshua awambie hao watu yakaisha, sawasawa na hayo yote Musa aliyokuwa amemwamuru Yoshua; kisha hao watu wakafanya haraka wakavuka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wale makuhani waliobeba sanduku la agano, walisimama katikati ya mto Yordani mpaka watu walipomaliza kutekeleza kila kitu ambacho Mwenyezi-Mungu alimwamuru Yoshua awaambie watu; Yoshua alifanya yote ambayo Mose alikuwa amemwamuru. Watu wakaharakisha kuvuka mto,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini watambikaji waliolichukua hilo Sanduku walikuwa wanasimama katikati ya Yordani, mpaka mambo yote yakamalizika, Bwana aliyomwagiza Yosua kuwaambia watu, nayo yalikuwa sawa na yale, Mose aliyomwagiza Yosua. Nao watu wakavuka mbiombio.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa makuhani waliolichukua hilo sanduku walisimama katikati ya Yordani, hata mambo yote BWANA aliyomwamuru Yoshua awambie hao watu yakaisha, sawasawa na hayo yote Musa aliyokuwa amemwamuru Yoshua; kisha hao watu wakafanya haraka wakavuka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wale makuhani waliobeba Sanduku la Agano, walisimama katikati ya muto Yordani mpaka watu walipomaliza kutimiza kila kitu ambacho Yawe alimwamuru Yoshua awaambie watu; Yoshua alifanya yote ambayo Musa alikuwa amemwamuru. Watu wakaharakisha kuvuka muto,