Joshua 4:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hao makuhani waliokuwa wamebeba lile sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu walipotoka katikati ya mto Yordani, na kukanyaga ukingo wa mto, maji ya mto Yordani yakaanza kutiririka tena, na kufurika kama kwanza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nao makuhani wakapanda kutoka ndani ya Mto Yordani wakilibeba hilo Sanduku la Agano la Mwenyezi Mungu. Mara tu walipoiweka miguu yao ukingoni mwa mto, maji ya Yordani yakarudi kufurika kama ilivyokuwa kabla.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ilikuwa, hapo hao makuhani waliolichukua sanduku la agano la Bwana walipokwea juu kutoka mle kati ya Yordani, na nyayo za miguu yao hao makuhani zilipoinuliwa na kutiwa katika nchi kavu, ndipo maji ya Yordani yaliporudi mahali pake, na kujaa na kuipita mipaka yake, kama yalivyokuwa hapo kwanza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hao makuhani waliokuwa wamebeba lile sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu walipotoka katikati ya mto Yordani, na kukanyaga ukingo wa mto, maji ya mto Yordani yakaanza kutiririka tena, na kufurika kama kwanza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nao makuhani wakapanda kutoka ndani ya Mto Yordani wakilibeba hilo Sanduku la Agano la BWANA. Mara walipoiweka miguu yao penye kingo, nje ya mto, maji ya Yordani yakarudi kufurika kama ilivyokuwa kabla.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nao makuhani wakapanda kutoka ndani ya Mto Yordani wakilibeba hilo Sanduku la Agano la bwana. Mara tu walipoiweka miguu yao penye kingo, nje ya mto, maji ya Yordani yakarudi kufurika kama ilivyokuwa kabla.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ilikuwa, hapo hao makuhani waliolichukua sanduku la Agano la BWANA walipokwea juu kutoka mle kati ya Yordani, na nyayo za miguu yao hao makuhani zilipoinuliwa na kutiwa katika nchi kavu, ndipo maji ya Yordani yaliporudi mahali pake, na kufurika katika kingo zake zote, kama yalivyokuwa hapo kwanza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hao makuhani waliokuwa wamebeba lile sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu walipotoka katikati ya mto Yordani, na kukanyaga ukingo wa mto, maji ya mto Yordani yakaanza kutiririka tena, na kufurika kama kwanza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa, watambikaji waliolichukua Sanduku la Agano la Bwana walipopanda na kutoka katikati ya Yordani, basi, nyayo za miguu ya hao watambikaji zilipoinuliwa kukanyaga pakavu, ndipo, maji ya Yordani yaliporudi mahali pao kuishika njia yao kama siku zote mpaka juu ukingoni pande zote mbili.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ilikuwa, hapo hao makuhani waliolichukua sanduku la agano la BWANA walipokwea juu kutoka mle kati ya Yordani, na nyayo za miguu yao hao makuhani zilipoinuliwa na kutiwa katika nchi kavu, ndipo maji ya Yordani yaliporudi mahali pake, na kujaa na kuipita mipaka yake, kama yalivyokuwa hapo kwanza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hao makuhani waliokuwa wanabeba lile Sanduku la Agano la Yawe walipotoka katikati ya muto Yordani, na kukanyaga ukingo wa muto, maji ya muto Yordani yakaanza kutiririka tena, na kufurika kama mbele.