Joshua 4:23 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtawaambia kuwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, aliyakausha maji ya mto Yordani kwa ajili yenu mpaka mkavuka, kama alivyokausha bahari ya Shamu, kwa ajili yetu tukavuka,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, alikausha maji ya Yordani mbele yenu, hadi mlipomaliza kuvuka. Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, alifanya haya kwa Mto Yordani sawasawa na kile alichoifanyia Bahari ya Shamu alipoikausha mbele yetu hadi tulipomaliza kuvuka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu Bwana, Mungu wenu aliyakausha maji ya Yordani, mbele yenu, hata mlipokwisha kuvuka kama Bwana, Mungu wenu, alivyoitenda Bahari ya Shamu, aliyoikausha mbele yetu hata tulipokwisha kuvuka;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtawaambia kuwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, aliyakausha maji ya mto Yordani kwa ajili yenu mpaka mkavuka, kama alivyokausha bahari ya Shamu, kwa ajili yetu tukavuka,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana BWANA Mungu wenu alikausha maji ya Yordani mbele yenu, hadi mlipomaliza kuvuka. BWANA Mungu wenu alifanya haya kwa Mto Yordani sawasawa na kile alichoifanyia Bahari ya Shamu wakati alipoikausha mbele yetu hadi tulipomaliza kuvuka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana bwana Mwenyezi Mungu wenu alikausha maji ya Yordani mbele yenu, hadi mlipomaliza kuvuka. bwana Mwenyezi Mungu wenu alifanya haya kwa Mto Yordani sawasawa na kile alichoifanyia Bahari ya Shamu wakati alipoikausha mbele yetu hadi tulipomaliza kuvuka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa sababu BWANA, Mungu wenu aliyakausha maji ya Yordani, mbele yenu, hadi mlipokwisha kuvuka kama BWANA, Mungu wenu, alivyoitenda Bahari ya Shamu, aliyoikausha mbele yetu hata tulipokwisha kuvuka;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtawaambia kuwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, aliyakausha maji ya mto Yordani kwa ajili yenu mpaka mkavuka, kama alivyokausha bahari ya Shamu, kwa ajili yetu tukavuka,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kwa kuwa Bwana Mungu wenu aliyapwesha maji ya Yordani mbele yenu, mpaka mwishe kuvuka, kama Bwana Mungu wenu alivyofanya penye Bahari Nyekundu, alipoipwesha mbele yetu, mpaka tuishe kuvuka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu BWANA, Mungu wenu aliyakausha maji ya Yordani, mbele yenu, hata mlipokwisha kuvuka kama BWANA, Mungu wenu, alivyoitenda Bahari ya Shamu, aliyoikausha mbele yetu hata tulipokwisha kuvuka;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutawaambia kwamba Yawe, Mungu wenu, aliyakausha maji ya muto Yordani kwa ajili yenu mpaka mukavuka, kama vile alivyofanya kwa bahari Nyekundu. Akaikausha mbele yetu mpaka tulipovuka