Joshua 4:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
uwaagize hivi, ‘Chukueni mawe kumi na mawili kutoka hapa katikati ya mto Yordani, kutoka hapa ilipo miguu ya makuhani, muyachukue mawe hayo, mkayaweke mahali pale ambapo mtalala leo hii.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
uwaambie wachukue mawe kumi na mbili katikati ya Mto Yordani, pale makuhani waliposimama, wayachukue na kuyaweka mahali mtakapokaa usiku huu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kisha uwaamrishe, kusema, Twaeni mawe kumi na mawili, hapo katikati ya Yordani, mahali hapo miguu ya hao makuhani iliposimama imara, mwende nayo mawe hayo, mkayaweke nchi kambini, hapo mtakapolala usiku huu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
uwaagize hivi, ‘Chukueni mawe kumi na mawili kutoka hapa katikati ya mto Yordani, kutoka hapa ilipo miguu ya makuhani, muyachukue mawe hayo, mkayaweke mahali pale ambapo mtalala leo hii.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
nawe uwaambie wachukue mawe kumi na mawili katikati ya Mto Yordani, pale pale makuhani waliposimama, wayachukue na kuyaweka mahali mtakapokaa usiku huu wa leo.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
nawe uwaambie wachukue mawe kumi na mawili katikati ya Mto Yordani, palepale makuhani waliposimama, wayachukue na kuyaweka mahali mtakapokaa usiku huu wa leo.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kisha uwaamrishe, kusema, Twaeni mawe kumi na mawili, hapo katikati ya Yordani, mahali hapo miguu ya hao makuhani iliposimama imara, mwende na mawe hayo, mkayaweke mahali pale kambini ambapo mtalala usiku huu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
uwaagize hivi, ‘Chukueni mawe kumi na mawili kutoka hapa katikati ya mto Yordani, kutoka hapa ilipo miguu ya makuhani, muyachukue mawe hayo, mkayaweke mahali pale ambapo mtalala leo hii.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha waagizeni kwamba: Chukueni katikati ya Yordani hapo, watambikaji waliposimama na kuishikiza miguu, mawe kumi na mawili, myapitishe mtoni kwenda nayo, myapeleke kambini, mtakakolala usiku huu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kisha uwaamrishe, kusema, Twaeni mawe kumi na mawili, hapo katikati ya Yordani, mahali hapo miguu ya hao makuhani iliposimama imara, mwende nayo mawe hayo, mkayaweke nchi kambini, hapo mtakapolala usiku huu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
uwaagize hivi: ‘Mutwae mawe kumi na mawili kutoka hapa katikati ya muto Yordani, kutoka hapa miguu ya makuhani ilipokuwa, mutwae mawe hayo, muyaweke pahali pale ambapo mutalala leo hii.’ ”