Joshua 4:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
akawaambia, “Litangulieni sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mpaka katikati ya mto Yordani. Kila mmoja wenu achukue jiwe begani mwake, jiwe moja kwa ajili ya kila kabila la Israeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
naye akawaambia, “Mtangulie mbele ya Sanduku la Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, mwende katikati ya Mto Yordani. Kila mmoja wenu atainua jiwe begani mwake, kulingana na idadi ya makabila ya Israeli,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
naye Yoshua akawaambia, Haya, piteni ninyi mtangulie mbele ya sanduku la Bwana, Mungu wenu, mwende pale katikati ya Yordani, mkatwae kila mtu wenu jiwe moja begani mwake, kwa kadiri ya hesabu ya kabila za wana wa Israeli;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
akawaambia, “Litangulieni sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mpaka katikati ya mto Yordani. Kila mmoja wenu achukue jiwe begani mwake, jiwe moja kwa ajili ya kila kabila la Israeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
naye akawaambia, “Mtangulie mbele ya Sanduku la BWANA Mungu wenu, mwende katikati ya Mto Yordani. Kila mmoja wenu atainua jiwe begani mwake, kufuatana na hesabu ya makabila ya Waisraeli,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
naye akawaambia, “Mtangulie mbele ya Sanduku la bwana Mwenyezi Mungu wenu, mwende katikati ya Mto Yordani. Kila mmoja wenu atainua jiwe begani mwake, kufuatana na hesabu ya makabila ya Waisraeli,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
naye Yoshua akawaambia, Haya, piteni ninyi mtangulie mbele ya sanduku la BWANA, Mungu wenu, mwende pale katikati ya Yordani, mkatwae kila mmoja wenu jiwe moja begani mwake, kwa kadiri ya hesabu ya makabila ya wana wa Israeli;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
akawaambia, “Litangulieni sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mpaka katikati ya mto Yordani. Kila mmoja wenu achukue jiwe begani mwake, jiwe moja kwa ajili ya kila kabila la Israeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kisha Yosua akawaambia: Nendeni mbele penye Sanduku la Bwana Mungu wenu lililoko katikati ya Yordani, mjitwike kila mtu jiwe moja begani pake kwa hesabu ya mashina ya wana wa Isiraeli,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
naye Yoshua akawaambia, Haya, piteni ninyi mtangulie mbele ya sanduku la BWANA, Mungu wenu, mwende pale katikati ya Yordani, mkatwae kila mtu wenu jiwe moja begani mwake, kwa kadiri ya hesabu ya kabila za wana wa Israeli;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
akawaambia: “Mulitangulie Sanduku la Agano la Yawe, Mungu wenu, mpaka katikati ya muto Yordani. Kila mumoja wenu abebe jiwe kwenye bega lake, jiwe moja kwa ajili ya kila kabila la Israeli.