Joshua 4:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yoshua akasimika pia mawe kumi na mawili katikati ya mto Yordani, mahali pale ambapo nyayo za makuhani waliobeba lile sanduku la agano zilisimama. Mawe hayo yako huko mpaka hivi leo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yoshua akayasimamisha yale mawe kumi na mbili yaliyokuwa katikati ya Mto Yordani, mahali miguu ya makuhani waliobeba Sanduku la Agano iliposimama. Nayo yako huko hadi leo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha Yoshua akapanga mawe kumi na mawili katikati ya Yordani, mahali pale miguu ya hao makuhani waliolichukua hilo sanduku la agano iliposimama; nayo yapo pale pale hata hivi leo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yoshua akasimika pia mawe kumi na mawili katikati ya mto Yordani, mahali pale ambapo nyayo za makuhani waliobeba lile sanduku la agano zilisimama. Mawe hayo yako huko mpaka hivi leo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yoshua akayasimamisha yale mawe kumi na mawili ambayo yalikuwa katikati ya Mto Yordani, mahali pale ambapo miguu ya makuhani waliobeba Sanduku la Agano iliposimama. Nayo yako huko mpaka leo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yoshua akayasimamisha yale mawe kumi na mawili ambayo yalikuwa katikati ya Mto Yordani, mahali pale ambapo miguu ya makuhani waliobeba Sanduku la Agano iliposimama. Nayo yako huko mpaka leo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha Yoshua akapanga mawe kumi na mawili katikati ya Yordani, mahali pale miguu ya hao makuhani waliolichukua hilo sanduku la Agano iliposimama; nayo yapo pale pale hata hivi leo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yoshua akasimika pia mawe kumi na mawili katikati ya mto Yordani, mahali pale ambapo nyayo za makuhani waliobeba lile sanduku la agano zilisimama. Mawe hayo yako huko mpaka hivi leo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mawe kumi na mawili mengine Yosua akayasimika katikati ya Yordani hapo chini, watambikaji waliolichukua Sanduku la Agano walipoishikiza miguu yao, nayo yako huko mpaka siku hii ya leo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha Yoshua akapanga mawe kumi na mawili katikati ya Yordani, mahali pale miguu ya hao makuhani waliolichukua hilo sanduku la agano iliposimama; nayo yapo pale pale hata hivi leo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yoshua akasimika vilevile mawe kumi na mawili katikati ya muto Yordani, pahali pale miguu ya makuhani waliobeba lile Sanduku la Agano iliposimama. Mawe hayo yako kule mpaka hivi leo.