Joshua 5:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku moja Yoshua alipokuwa karibu na mji wa Yeriko, ghafla aliona mtu mmoja amesimama mbele yake na upanga uliofutwa mkononi mwake. Yoshua akamwendea, akamwuliza, “Je, wewe ni wetu au ni wa adui zetu?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Yoshua alipokuwa karibu na Yeriko, akainua macho, akaona mtu aliyesimama mbele yake, akiwa na upanga mkononi. Yoshua akamwendea na kumuuliza, “Je, wewe uko upande wetu au upande wa adui zetu?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa hapo Yoshua alipokuwa karibu na mji wa Yeriko, akavua macho yake na kuangalia, na tazama, mtu mume akasimama kumkabili mbele yake, naye alikuwa na upanga wazi mkononi mwake; Yoshua akamwendea, na kumwambia, Je! Wewe u upande wetu, au upande wa adui zetu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku moja Yoshua alipokuwa karibu na mji wa Yeriko, ghafla aliona mtu mmoja amesimama mbele yake na upanga uliofutwa mkononi mwake. Yoshua akamwendea, akamwuliza, “Je, wewe ni wetu au ni wa adui zetu?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi wakati Yoshua alipokaribia Yeriko, akainua macho, akaona mtu aliyesimama mbele yake, akiwa na upanga mkononi uliofutwa kwenye ala. Yoshua akamwendea na kumwuliza, “Je, wewe uko upande wetu au upande wa adui zetu?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi wakati Yoshua alipokuwa karibu na Yeriko, akainua macho, akaona mtu aliyesimama mbele yake, akiwa na upanga mkononi uliofutwa kwenye ala. Yoshua akamwendea na kumuuliza, “Je, wewe uko upande wetu au upande wa adui zetu?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa hapo Yoshua alipokuwa karibu na mji wa Yeriko, akainua macho yake na kuangalia juu, akaona ghafla mtu mmoja, mwanamume amesimama amemkabili naye alikuwa na upanga uliofutwa mkononi mwake; Yoshua akamwendea, na kumwambia, Je! Wewe u upande wetu, au upande wa adui zetu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku moja Yoshua alipokuwa karibu na mji wa Yeriko, ghafla aliona mtu mmoja amesimama mbele yake na upanga uliofutwa mkononi mwake. Yoshua akamwendea, akamwuliza, “Je, wewe ni wetu au ni wa adui zetu?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa, Yosua alipokuwa huko karibu ya Yeriko, akayainua macho yake na kuchungulia, mara akaona mtu aliyesimama hapo na kumtazama, namo mkononi mwake alishika upanga uliokwisha kuchomolewa. Yosua alipomwendea na kumwuliza: Wewe u mtu wa kwetu au wa adui zetu?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa hapo Yoshua alipokuwa karibu na mji wa Yeriko, akavua macho yake na kuangalia, na tazama, mtu mume akasimama kumkabili mbele yake, naye alikuwa na upanga wazi mkononi mwake; Yoshua akamwendea, na kumwambia, Je! Wewe u upande wetu, au upande wa adui zetu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku moja Yoshua alipokuwa karibu na muji wa Yeriko, aliona kwa rafla mutu mumoja akisimama mbele yake na upanga uliochomolewa katika mukono wake. Yoshua akamwendea, akamwuliza: “Wewe ni wetu au ni wa waadui zetu?”