Joshua 5:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huyo kamanda wa jeshi la Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Vua viatu vyako kwa maana mahali unaposimama ni patakatifu.” Yoshua akafanya hivyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Jemadari wa jeshi la Mwenyezi Mungu akajibu, “Vua viatu vyako, kwa maana mahali uliposimama ni patakatifu.” Naye Yoshua akafanya hivyo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Huyo amiri wa jeshi la Bwana akamwambia Yoshua, Vua viatu vyako miguuni mwako; kwa kuwa mahali hapo usimamapo ni patakatifu. Yoshua akafanya vivyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huyo kamanda wa jeshi la Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Vua viatu vyako kwa maana mahali unaposimama ni patakatifu.” Yoshua akafanya hivyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Amiri jeshi wa jeshi la BWANA akajibu, “Vua viatu vyako, kwa maana mahali hapa unaposimama ni patakatifu.” Naye Yoshua akafanya hivyo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Jemadari wa jeshi la bwana akajibu, “Vua viatu vyako, kwa maana mahali hapa unaposimama ni patakatifu.” Naye Yoshua akafanya hivyo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Huyo kamanda wa jeshi la BWANA akamwambia Yoshua, Vua viatu vyako miguuni mwako; kwa kuwa mahali hapo usimamapo ni patakatifu. Yoshua akafanya hivyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huyo kamanda wa jeshi la Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Vua viatu vyako kwa maana mahali unaposimama ni patakatifu.” Yoshua akafanya hivyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye mkuu wa vikosi vya Bwana akamwambia Yosua: Vivue viatu miguuni pako! Kwani mahali hapa, wewe unaposimama, ndipo patakatifu. Yosua akafanya hivyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Huyo amiri wa jeshi la BWANA akamwambia Yoshua, Vua viatu vyako miguuni mwako; kwa kuwa mahali hapo usimamapo ni patakatifu. Yoshua akafanya vivyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Huyo jemadari wa jeshi la Yawe akamwambia: “Vua viatu vyako kwa maana pahali unaposimama ni patakatifu.” Yoshua akafanya hivyo.