Joshua 5:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sababu ya kuwatahiri Waisraeli ni hii: Waisraeli wote, wanaume, waliotoka Misri ambao walikuwa na umri wa kwenda vitani, wote walifariki safarini jangwani baada ya kutoka nchini Misri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hii ndiyo sababu ya Yoshua kufanya hivyo: Wanaume wote waliotoka Misri, wote wenye umri wa kwenda vitani, walikufa jangwani wakiwa njiani baada ya kuondoka Misri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na sababu ya Yoshua kutahiri ni hii; watu wote waliotoka Misri, waliokuwa waume, hao watu waume wote waendao vitani walikufa katika bara njiani, baada ya wao kutoka Misri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sababu ya kuwatahiri Waisraeli ni hii: Waisraeli wote, wanaume, waliotoka Misri ambao walikuwa na umri wa kwenda vitani, wote walifariki safarini jangwani baada ya kutoka nchini Misri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hii ndiyo sababu ya kufanya hivyo: Wanaume wote waliotoka Misri, wote wenye umri wa kwenda vitani, walikufa jangwani wakiwa njiani, baada ya kuondoka Misri.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hii ndiyo sababu ya Yoshua kufanya hivyo: Wanaume wote waliotoka Misri, wote wenye umri wa kwenda vitani, walikufa jangwani wakiwa njiani baada ya kuondoka Misri.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na sababu ya Yoshua kutahiri ni hii; watu wote wanaume waliotoka Misri, waliokuwa wapiganaji vita wote walifariki katika safari jangwani baada ya kutoka Misri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sababu ya kuwatahiri Waisraeli ni hii: Waisraeli wote, wanaume, waliotoka Misri ambao walikuwa na umri wa kwenda vitani, wote walifariki safarini jangwani baada ya kutoka nchini Misri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena sababu yake Yosua ya kuwatahiri ilikuwa hii: watu wote waliotoka Misri waume wao wote walikuwa watu wa vita, nao walikufa nyikani njiani, walipokwisha kutoka Misri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na sababu ya Yoshua kutahiri ni hii; watu wote waliotoka Misri, waliokuwa waume, hao watu waume wote waendao vitani walikufa katika bara njiani, baada ya wao kutoka Misri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sababu ya kuwatahiri Waisraeli ni hii: Waisraeli wote, wanaume, waliotoka Misri ambao walikuwa na umri wa kwenda kwa vita, wote walikufa katika safari ndani ya jangwa nyuma ya kutoka katika inchi ya Misri.