Joshua 5:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waisraeli walisafiri kwa muda wa miaka arubaini nyikani hata wanaume wote waliokuwa na umri wa kwenda vitani wakaangamia kwa kuwa hawakusikiliza aliyosema Mwenyezi-Mungu. Mwenyezi-Mungu alikuwa amewaapia watu hao kwamba hawataiona nchi ile inayotiririka maziwa na asali ambayo yeye aliwaapia baba zao kuwa atawapa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waisraeli walitembea jangwani miaka arobaini hadi wanaume wote wale waliokuwa na umri wa kwenda vitani wakati waliondoka Misri walipokwisha kufa, kwa kuwa hawakumtii Mwenyezi Mungu. Kwa maana Mwenyezi Mungu alikuwa amewaapia kuwa wasingeweza kuona nchi ambayo alikuwa amewaahidi baba zao katika kuapa kutupatia, nchi inayotiririka maziwa na asali.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa wana wa Israeli walitembea muda wa miaka arobaini barani, hata hilo taifa zima, yaani, watu waume waendao vitani, waliotoka Misri, walipokuwa wameangamia; kwa sababu hawakuisikiza sauti ya Bwana; nao ndio Bwana aliowaapia ya kwamba hatawaacha waione hiyo nchi, ambayo Bwana aliwaapia baba zao kwamba atatupa sisi; nchi ijaayo maziwa na asali.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waisraeli walisafiri kwa muda wa miaka arubaini nyikani hata wanaume wote waliokuwa na umri wa kwenda vitani wakaangamia kwa kuwa hawakusikiliza aliyosema Mwenyezi-Mungu. Mwenyezi-Mungu alikuwa amewaapia watu hao kwamba hawataiona nchi ile inayotiririka maziwa na asali ambayo yeye aliwaapia baba zao kuwa atawapa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Waisraeli walitembea jangwani miaka arobaini mpaka wanaume wote wale waliokuwa na umri wa kwenda vitani wakati walipoondoka Misri walipokwisha kufa, kwa kuwa hawakumtii BWANA. Kwa maana BWANA alikuwa amewaapia kuwa wasingeweza kuona nchi ambayo alikuwa amewaahidi baba zao kuwapatia, nchi inayotiririka maziwa na asali.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waisraeli walitembea jangwani miaka arobaini mpaka wanaume wote wale waliokuwa na umri wa kwenda vitani wakati waliondoka Misri walipokwisha kufa, kwa kuwa hawakumtii bwana. Kwa maana bwana alikuwa amewaapia kuwa wasingeweza kuona nchi ambayo alikuwa amewaahidi baba zao katika kuapa kutupatia, nchi inayotiririka maziwa na asali.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa wana wa Israeli walitembea muda wa miaka arobaini barani, hadi hilo taifa zima, yaani, watu wanaume wapiganaji vita, waliotoka Misri, walipokuwa wameangamia; kwa sababu hawakuisikiliza sauti ya BWANA; nao ndio BWANA aliowaapia ya kwamba hatawaacha waione hiyo nchi, ambayo BWANA aliwaapia baba zao kwamba atatupa sisi; nchi itiririkayo maziwa na asali.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waisraeli walisafiri kwa muda wa miaka arubaini nyikani hata wanaume wote waliokuwa na umri wa kwenda vitani wakaangamia kwa kuwa hawakusikiliza aliyosema Mwenyezi-Mungu. Mwenyezi-Mungu alikuwa amewaapia watu hao kwamba hawataiona nchi ile inayotiririka maziwa na asali ambayo yeye aliwaapia baba zao kuwa atawapa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani wana wa Isiraeli walizunguka nyikani miaka 40, mpaka wale watu wa vita wote pia waliotoka Misri walipokwisha kufa, kwa kuwa hawakuisikia sauti ya Bwana; kwa hiyo Bwana aliwaapia, wasiione ile nchi, yeye Bwana aliyowaapia baba zao, ya kama atatupa sisi, ni nchi hiyo inayochuruzika maziwa na asali.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa wana wa Israeli walitembea muda wa miaka arobaini barani, hata hilo taifa zima, yaani, watu waume waendao vitani, waliotoka Misri, walipokuwa wameangamia; kwa sababu hawakuisikiza sauti ya BWANA; nao ndio BWANA aliowaapia ya kwamba hatawaacha waione hiyo nchi, ambayo BWANA aliwaapia baba zao kwamba atatupa sisi; nchi ijaayo maziwa na asali.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waisraeli walisafiri kwa muda wa miaka makumi ine katika jangwa hata wanaume wote waliokuwa na umri wa kwenda kwa vita wakaangamia kwa kuwa hawakusikiliza mambo Yawe aliyosema. Yawe alikuwa amewaapia watu hao kwamba hawataiona inchi ile inayotiririka maziwa na asali ambayo yeye aliwaapia baba zao kwamba atawapa.