Joshua 6:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Yoshua akawaamuru watu, “Msipige kelele au kutoa sauti, wala neno lolote lisitoke vinywani mwenu, mpaka siku ile ambapo nitawaambieni mpige kelele; wakati huo ndipo mtakapopiga kelele.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Bali Yoshua alikuwa amewaagiza watu, “Msipige ukelele wa vita; msipaze sauti zenu, wala kusema neno lolote hadi siku ile nitakayowaambia mpige kelele. Ndipo mtapiga kelele!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yoshua akawaamuru watu, akasema Msipige kelele, wala sauti zenu zisisikiwe, wala neno lo lote lisitoke kinywani mwenu, hata siku ile nitakapowaamuru kupiga kelele, ndipo mtakapopiga kelele.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Yoshua akawaamuru watu, “Msipige kelele au kutoa sauti, wala neno lolote lisitoke vinywani mwenu, mpaka siku ile ambapo nitawaambieni mpige kelele; wakati huo ndipo mtakapopiga kelele.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Bali Yoshua aliwaagiza watu, “Msipige kelele za vita, msipaze sauti zenu, wala kusema neno lo lote mpaka siku ile nitakayowaambia mpige kelele. Ndipo mtapiga kelele!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Bali Yoshua alikuwa amewaagiza watu, “Msipige kelele ya vita, msipaze sauti zenu, wala kusema neno lolote mpaka siku ile nitakayowaambia mpige kelele. Ndipo mtapiga kelele!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yoshua akawaamuru watu, akasema Msipige kelele, wala sauti zenu zisisikiwe, wala neno lolote lisitoke kinywani mwenu, hadi siku ile nitakapowaamuru kupiga kelele, ndipo mtakapopiga kelele.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Yoshua akawaamuru watu, “Msipige kelele au kutoa sauti, wala neno lolote lisitoke vinywani mwenu, mpaka siku ile ambapo nitawaambieni mpige kelele; wakati huo ndipo mtakapopiga kelele.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini wale watu Yosua alikuwa amewaagiza kwamba: Msizomee! Wala sauti zenu zisisikilike! Wala neno lo lote lisitoke vinywani mwenu mpaka ile siku, nitakayowaambia: Zomeeni! Hapo ndipo, mtakapozomea.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yoshua akawaamuru watu, akasema Msipige kelele, wala sauti zenu zisisikiwe, wala neno lo lote lisitoke kinywani mwenu, hata siku ile nitakapowaamuru kupiga kelele, ndipo mtakapopiga kelele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Yoshua akawaamuru watu: “Musipige kelele au kutoa sauti, wala neno lolote lisitoke katika vinywa vyenu, mpaka siku ile ambapo nitawaambia mupige kelele; wakati ule ndipo mutakapopiga kelele.”