Joshua 6:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wale makuhani saba wenye mabaragumu saba za kondoo dume walitembea mbele ya sanduku la Mwenyezi-Mungu wakipiga mabaragumu mfululizo. Watu wenye silaha walilitangulia sanduku la Mwenyezi-Mungu na walinzi wengine nyuma yake. Mabaragumu yakaendelea kupigwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale Makuhani saba waliobeba zile baragumu saba wakatangulia mbele ya Sanduku la Mwenyezi Mungu wakizipiga. Watu wenye silaha wakatangulia mbele yao na walinzi wa nyuma wakalifuata Sanduku la Mwenyezi Mungu, huku baragumu hizo zikiendelea kulia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na wale makuhani saba wakazichukua tarumbeta saba za pembe za kondoo waume mbele ya sanduku la Bwana, wakaendelea wakazipiga tarumbeta; nao watu wenye silaha wakawatangulia, na hao waliokuwa nyuma wakalifuata sanduku la Bwana; makuhani wakizipiga tarumbeta walipokuwa wakienda.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wale makuhani saba wenye mabaragumu saba za kondoo dume walitembea mbele ya sanduku la Mwenyezi-Mungu wakipiga mabaragumu mfululizo. Watu wenye silaha walilitangulia sanduku la Mwenyezi-Mungu na walinzi wengine nyuma yake. Mabaragumu yakaendelea kupigwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Makuhani saba wakachukua zile baragumu saba wakatangulia mbele ya Sanduku la BWANA wakizipiga hizo baragumu. Watu wenye silaha wakatangulia mbele yao, walinzi waliokuwa nyuma wakalifuata Sanduku la BWANA, huku makuhani wakiendelea kuzipiga hizo baragumu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wale Makuhani saba wakizibeba zile baragumu saba wakatangulia mbele ya Sanduku la bwana wakizipiga. Watu wenye silaha wakatangulia mbele yao na walinzi wa nyuma wakalifuata Sanduku la bwana, huku baragumu hizo zikiendelea kulia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na wale makuhani saba wakayachukua mabaragumu saba ya pembe za kondoo dume mbele ya sanduku la BWANA, wakaenda huku wakipiga mabaragumu; nao watu wenye silaha wakawatangulia, na hao waliokuwa nyuma wakalifuata sanduku la BWANA; huku makuhani wakipiga mabaragumu bila kukoma.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wale makuhani saba wenye mabaragumu saba za kondoo dume walitembea mbele ya sanduku la Mwenyezi-Mungu wakipiga mabaragumu mfululizo. Watu wenye silaha walilitangulia sanduku la Mwenyezi-Mungu na walinzi wengine nyuma yake. Mabaragumu yakaendelea kupigwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao wale watambikaji saba wakayachukua yale mabaragumu yenye milio mikubwa kwenda mbele ya Bwana; basi, walikuwa wanakwenda na kuyapiga hayo mabaragumu, nao wenye mata walikwenda mbele yao, nao wafuasi wa nyuma walikwenda nyuma ya Sanduku la Bwana; wote walikuwa wanakwenda, mabaragumu yakilia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na wale makuhani saba wakazichukua tarumbeta saba za pembe za kondoo waume mbele ya sanduku la BWANA, wakaendelea wakazipiga tarumbeta; nao watu wenye silaha wakawatangulia, na hao waliokuwa nyuma wakalifuata sanduku la BWANA; makuhani wakizipiga tarumbeta walipokuwa wakienda.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wale makuhani saba wenye mabaragumu saba ya kondoo dume walitembea mbele ya Sanduku la Yawe wakipiga mabaragumu kwa mufululizo. Watu wenye silaha walilitangulia Sanduku la Yawe na walinzi wengine nyuma yake. Mabaragumu yakaendelea kupigwa.