Joshua 6:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku ya saba, waliamka alfajiri na mapema, wakauzunguka mji huo mara saba kwa namna ileile. Ilikuwa ni siku hiyo tu ambayo waliuzunguka mji huo mara saba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku ya saba, wakaamka asubuhi na mapema wakauzunguka mji kama walivyokuwa wakifanya, isipokuwa siku ile waliuzunguka mji mara saba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa siku ya saba wakaondoka asubuhi na mapema wakati wa mapambazuko, wakauzunguka mji vivyo hivyo mara saba; ila siku hiyo waliuzunguka huo mji mara saba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku ya saba, waliamka alfajiri na mapema, wakauzunguka mji huo mara saba kwa namna ileile. Ilikuwa ni siku hiyo tu ambayo waliuzunguka mji huo mara saba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku ya saba, wakaamka asubuhi na mapema wakazunguka mji kama walivyokuwa wakifanya, isipokuwa siku ile waliuzunguka mji mara saba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku ya saba, wakaamka asubuhi na mapema wakauzunguka mji kama walivyokuwa wakifanya, isipokuwa siku ile waliuzunguka mji mara saba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa siku ya saba wakaondoka asubuhi na mapema wakati wa mapambazuko, wakauzunguka mji vivyo hivyo mara saba; ni siku hiyo tu ambapo waliuzunguka huo mji mara saba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku ya saba, waliamka alfajiri na mapema, wakauzunguka mji huo mara saba kwa namna ileile. Ilikuwa ni siku hiyo tu ambayo waliuzunguka mji huo mara saba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku ya saba wakaamka asubuhi, mapambazuko yalipoanza, wakauzunguka huo mji mara saba vivyo hivyo, kama walivyofanya siku zote; lakini siku hiyo wakauzunguka huo mji mara saba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa siku ya saba wakaondoka asubuhi na mapema wakati wa mapambazuko, wakauzunguka mji vivyo hivyo mara saba; ila siku hiyo waliuzunguka huo mji mara saba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku ya saba, waliamuka asubui mapema, wakauzunguka muji ule mara saba. Ilikuwa ni siku hiyo tu ambayo waliuzunguka muji ule mara saba.