Joshua 6:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ilipofika mara ya saba, wakati makuhani walipokwisha piga mabaragumu, Yoshua akawaambia watu, “Pigeni kelele, kwa kuwa Mwenyezi-Mungu amekwisha wapeni huu mji!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walipouzunguka mara ya saba, makuhani walipiga baragumu kwa sauti kubwa, naye Yoshua akawaamuru watu akisema, “Pigeni kelele! Kwa maana Mwenyezi Mungu amewapa mji huu!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata mara ya saba makuhani walipozipiga tarumbeta, Yoshua akawaambia watu, Pigeni kelele; kwa maana Bwana amewapeni mji huu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ilipofika mara ya saba, wakati makuhani walipokwisha piga mabaragumu, Yoshua akawaambia watu, “Pigeni kelele, kwa kuwa Mwenyezi-Mungu amekwisha wapeni huu mji!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walipouzunguka mara ya saba, makuhani walipopiga baragumu kwa sauti kubwa, Yoshua akawaamuru watu akisema, “Pigeni kelele! Kwa maana BWANA amewapa mji huu!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walipouzunguka mara ya saba, makuhani walipopiga baragumu kwa sauti kubwa, Yoshua akawaamuru watu akisema, “Pigeni kelele! Kwa maana bwana amewapa mji huu!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata mara ya saba makuhani wakapiga mabaragumu, Yoshua akawaambia watu, Pigeni kelele; kwa maana BWANA amewapeni mji huu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ilipofika mara ya saba, wakati makuhani walipokwisha piga mabaragumu, Yoshua akawaambia watu, “Pigeni kelele, kwa kuwa Mwenyezi-Mungu amekwisha wapeni huu mji!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ilipofika mara ya saba, watambikaji wale walipoyapiga mabaragumu, ndipo, Yosua alipowaambia watu: Zomeeni! Kwani Bwana amewapa mji huu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata mara ya saba makuhani walipozipiga tarumbeta, Yoshua akawaambia watu, Pigeni kelele; kwa maana BWANA amewapeni mji huu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ilipofika mara ya saba, wakati makuhani walipokwisha kupiga mabaragumu, Yoshua akawaambia watu: “Mupige kelele, kwa kuwa Yawe amekwisha kuwapa huu muji!