Joshua 6:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini msichukue chochote ambacho kimewekwa wakfu ili kiangamizwe, mkichukua kitu chochote ambacho kimewekwa wakfu ili kiangamizwe mtaifanya kambi ya Israeli kuwa kitu cha kuangamizwa, na hivyo kuiletea balaa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini mjiepushe na vitu vilivyotengwa kwa ajili ya kuangamizwa, msije mkajiletea maangamizi kwa kuchukua chochote katika hivyo; la sivyo, mtailetea kambi ya Israeli maangamizi na taabu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na ninyi, msikose kujiepusha na kitu kilichowekwa wakfu; msije mkakitwaa kitu kilichowekwa wakfu, baada ya kukiweka wakfu; nanyi hivyo mtayafanya matuo ya Israeli kuwa yamelaaniwa na kuyafadhaisha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini msichukue chochote ambacho kimewekwa wakfu ili kiangamizwe, mkichukua kitu chochote ambacho kimewekwa wakfu ili kiangamizwe mtaifanya kambi ya Israeli kuwa kitu cha kuangamizwa, na hivyo kuiletea balaa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini mjiepushe na vitu vilivyowekwa wakfu, msije mkachukua cho chote katika hivyo, msije mkajiletea maangamizi katika maskani ya Israeli na kuiletea taabu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini mjiepushe na vitu vilivyowekwa wakfu, msije mkachukua chochote katika hivyo, msije mkajiletea maangamizi katika maskani ya Israeli na kuiletea taabu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na ninyi, msikose kujiepusha na kitu kilichowekwa wakfu; msije mkakitwaa kitu kilichowekwa wakfu, baada ya kukiweka wakfu; nanyi hivyo mtaifanya kambi ya Israeli kuwa imelaaniwa na kuifadhaisha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini msichukue chochote ambacho kimewekwa wakfu ili kiangamizwe, mkichukua kitu chochote ambacho kimewekwa wakfu ili kiangamizwe mtaifanya kambi ya Israeli kuwa kitu cha kuangamizwa, na hivyo kuiletea balaa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jiangalieni sana kwa ajili yao yaliyo yenye mwiko, msiyatie kwanza mwiko, kisha mkachukua mengine yaliyo yenye mwiko. Kwani hivyo mtayapatia makambi ya Waisiraeli viapizo kwa kuyaponza
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na ninyi, msikose kujiepusha na kitu kilichowekwa wakfu; msije mkakitwaa kitu kilichowekwa wakfu, baada ya kukiweka wakfu; nanyi hivyo mtayafanya matuo ya Israeli kuwa yamelaaniwa na kuyafadhaisha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini musitwae kitu chochote ambacho kimetolewa kusudi kiangamizwe. Mukitwaa kitu chochote ambacho kimetolewa kusudi kiangamizwe, mutaifanya kambi ya Israeli kuwa kitu cha kuangamizwa, na hivyo kuiletea hasara.